…………………………………………………………………………………………………….
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wabunge wa Tanzania
kwenye bunge la Afrika mashariki wametoka nje ya bunge akigomea kuletwa
kwa muswada wa mabadiliko ya sheria za bandari ambao hauna maslahi na
taifa letu.
Akiongea nje ya
ukumbi wa bunge hilo Mariamu Ussi Yahaya alisema kuwa muswada huo
unaotakiwa kuletwa utaounguza mapato ya bandari zetu hivyo hauna maslahi
kwa taifa letu.
Alieleza kuwa nchi
zenye bandari kwenye jumuiya hiyo ni Tanzania na Kenya hivyo kuletwa
kwake ndani ya bunge kwa wakati huu sio sahihi una lengo la kuhujumu
mapato yetu kama taifa
Aliwambia kuwa
Hatukatai muswada huu kama nchi kwa kuwa bado kuna takiwa kufanyika kwa
mapitio na upembuzi kabla haujaletwa bungeni kujadiliwa lakini tunaona
unataka kuletwa bunge kabla haujafanyiwa upembuzi kwani sheria hii
ilikuwepo awali.
“Tumeamua kutoka nje
baada ya kuona Kuna muswada wa sheria ambao hauna nia nzuri kwani sheria
zipo na zinaweza kubadilishwa lakini sio kwa wakati huu”
Muswada mbalimbali
imajadiliwa tokea kuanza kwa bunge hilo wiki iliyopita ikiwemo kusomwa
kwa taarifa ya ukaguzi wa fedha za jumuiya hiyo iliyowasilishwa bungeni
humo na mbunge na Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ya bunge hilo Dkt.Ngwaru
Maghembe na kueleza kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa tofauti na mwaka
uliopita kwenye matumizi ya jumuiya.
Hali hiyo imeonyesha
kuongezeka kwa ubanaji wa matumizi ya shughuli za jumuiya hiyo kama
agizo la Mwenyekiti wa wakati huo Dkt.John Magufuli alivyoahidi hali
hiyo imepelekea mwaka huu jumuiya hiyo kupata hati safi tofauti na mwaka
uliopita.
Bunge hilo
linalotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu tarehe 29 limekuwa na
mijadala mikali inayoendelea hali iliyopelekea Jana wabunge watanzania
kutoka nje ya ukumbi wakigomea kuletwa kwa muswada wa mabadiliko ya
sheria za bandari ambazo wao wanaona hazina maslahi mazuri na kwa taifa
na itapunguza mapato ya bandari zetu.
No comments:
Post a Comment