Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mhe.William Ole Nasha akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa
Vitabu uliofanyika katika ofisi ya Taasisi ya Elimu Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akizungumza katika hafla ya
Uzinduzi wa Vitabu uliofanyika katika ofisi ya Taasisi ya Elimu Jijini
Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mhe.William Ole Nasha akizindua vitabu vya kiada na
kusambazwa katika shule mbalimbali Tanzania bara na Visiwani kwaajili ya
matumizi ya ksoma na kufundishia.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mhe.William Ole Nasha akiwa kwenye picha ya pampja na wadau
mbalimbali wa elimu baada ya haflaya uzinduzi wa vitabu vya kiada na
kusambazwa katika shule mbalimbali Tanzania bara na Visiwani kwaajili ya
matumizi ya kusoma na kufundishia.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Mhe.William Ole Nasha akikagua vitabu ambavyo vitatumika
kwaajili ya kusoma na kufundishia shuleni.
***************************
NA EMMANUEL MBATILO
Serikali haitaruhusu kuuza na
kusumbaza vitabu vyote vya elimu vya kiada na ziada visivyo na
ithibati
na yeyote atakaye kiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria
ili kuhakikisha maudhui ya elimu wanayoipitia wanafunzi yanakuwa bora
nayakukidhi viwango vilivyo bora.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es
Salaam Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha
katika hafla ya uzinduzi wa kazi ya usambazaji wa vitabu vya kiada.
Aidha Mhe.Ole Nasha amesema vitabu
ni nyenzo muhimu katika sekta ya elimu hivyo ameitaka taasisi ya elimu
nchini kuongeza juhudu katika umalaziaji wa mchakato wa uandaaji vitabu
kwa darasa la sita na la saba ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu
bora.
“Unaweza ukafanya chochote katika
elimu, unaweza kujenga majengo, kuajiri walimu lakini vitabu vya kiada
na ziada ndio moyo wa elimu pasipo kuwanavyo juhudi zote zinazofanywa ni
bure”. Amesema Mh.Ole Nasha.
Ameongeza kuwa serikali inalidhia
kuhakikisha sera ya elimu inatimizwa kikamlifu kwa kuwapatia elimu bora
watoto wote pasipokujali changamoto ambapo wanafunzi wenye ulemavu wa
kutokuona watapatiwa kitabu kimoja cha nukta nundu kwa kila mwanufunzi
huku wenye mahitaji maalumu wakitumia kitabu kimoja wanafunzi watatu.
Pamoja na hayo Mhe.Ole Nasha
amewataka wasambazaji na wauzaji wa vitabu vya kiada na ziada vya ngazi
mbalimbli za elimu nchini kuacha kuuza na kusambaza vitabu visivyo na
ithibati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Taasisi ya Elimu Tanzania, Dkt.Aneth Kombo amesema kuwa kupitia ufadhili
wa GPE LANES, taasisi hiyo imekamilisha kazi ya uandishi wa vitabu vya
nukta nundu na maandishi makubwa kwa darasa la I,II, na V. Vitabu hivyo
ni mahususi kwa matumizi ya wanafunzi wasiona na wale wenye uoni hafifu.
Dkt.Aneth amesema kuwa Jumla ya nakala 38,200 zitasambazwa kwa uwiano wa kitabu kimoja mwanafunzi mmoja.
Mwaka 2019 Taasisi ilichapa na
kusambaza vitabu kwa darasa la III na IV na jumla ya nakala 14,904 ya
vitabu vya nukta nundu na maandishi makubwa zilisambazwa kwa uwiano 1:1.
“Kwasasa Taasisi itanedelea
kukamilisha vitabu vya aina hiyo kwa darasa la VI na VII.Tunawashukuru
sana washirika wa maendeleo GPE LANELS kwa kufadhili kazi hii”. Amesema
Dkt.Aneth.
Pamoja na hayo Dkt.Aneth ameeleza
kuwa Taasisi hiyo imeshirikiana na shirika la SILOAM lililopo nchini
Korea linalojulikana kwa jina la SILOAM CENTER for the Blind kubadilisha
vitabu vya ziada vya kawaida kwa ngazi ya Elimu ya sekondari kuwa nukta
nundu.
“Shirika hili limefanya kazi ya
kubadilisha vitabu vya ziada vyenye idhini vya masomo ya Physics,
Chemistry, History,Civics, Biology,Kiswahili,Commerce na English kuanzia
kidato cha I-IV”. Ameeleza Dkt.Aneth.
Hata hivyo Dkt.Aneth amesema
vitabu vingine ni vya English Literature vya Wreath of Fr.Mayer,Pass
like a Shadow,Play this time tomorrow, The Interview,Growing up with
Poetry,Malenga Wapya,Ngoswe,Kilio Chetu, Wasaka Tonge, Houseboy, Three
Suitors one Husband,Selected Poems, Unnaswerd Cries,Song of Lawino and
Song of Okol.
No comments:
Post a Comment