Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linamshikilia ABRAHAM OBEDI [55] wakala wa bima ya GTM na Mkazi wa
Isanga Jijini Mbeya akiwa na mihuli sitini na sita [66] ya idara
mbalimbali za serikali na ofisi binafsi ambayo imeghushiwa na
kuhifadhiwa katika ofisi yake ya Stationaries.
Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31,
2019 majira ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya Mtaa wa Sokoine uliopo
Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani
hapa
kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa kumtia
nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.
Baadhi ya mihuli na nyaraka alizokutwa nazo mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-
- Mhuli wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,
- Mhuli wa Afisa biashara wa Halmashauri ya Mbeya,
- Access Bank Tawi la Mbeya,
- Mamlaka ya Mapato Mbeya [TRA],
- Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini.
Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na
Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima, Poss Machine na nyaraka
mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao vimeghushiwa. Upelelezi wa
shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
TAARIFA YA KUPATIKANA KWA WATOTO WAWILI WALIOKUWA WAMEPOTEA.
Mnamo tarehe 01.01.2020 huko Nzega
Mkoani Tabora, watoto wawili 1. FAISAL MASHAKA JUMA, miaka mitano na 2.
FARHANA JUMA, mwaka mmoja na miezi mitano waliokuwa wamepotea tangu
tarehe 28.12.2019 huko Ituha, Mtaa wa Shewa, Kata ya Mwakibete, Jijini
Mbeya wamepatikana wakiwa hai huko Mkoani Tabora. Jeshi la Polisi
linamshikilia mwanamke mmoja kuhusiana na tukio hilo. Upelelezi wa
shauri hili unaendelea.
No comments:
Post a Comment