Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Kijiji cha Mtipa 

Baadhi ya
wanufaika wa TASAF wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) alipowatembelea katika Halmashauri ya Manispaa ya
Singida, Kijiji cha Mtipa.

Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini Bi. Rebeca Mnyawi akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na
TASAF wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika
Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Kijiji cha Mtipa .

Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na baadhi ya walengwa wa TASAF
katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Kijiji cha Mtipa .

Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na mtoto wa Mnufaika wa TASAF
Bi.Tatu Salim wa Kijiji cha Mtipa katika Halmashauri ya Manispaa ya
Singida.

Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoka katika nyumba ya Mnufaika wa TASAF Bi.
Tatu Salim wa Kijiji cha Mtipa katika Halmashauri ya Manispaa ya
Singida alipomtembelea kukagua alivyonufaika na mradi wa TASAF.

Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa ameongozana na viongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Singida kukagua miradi ya TASAF katika Manispaa hiyo,
Kijiji cha Mtipa.

Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Mnufaika wa TASAF Bw. Issa Ramadhani alipomtembelea nyumbani kwake kukagua namna alivyonufaika na mradi huo.
……………………………………………
Na Happiness Shayo, Singida
Serikali imeweka mkakati wa
kuboresha huduma zinazotolewa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- ili...
ziweze kuwanufaisha zaidi Walengwa wa Mpango huo na hatimaye kupunguza umaskini nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika kijiji cha Mtipa,manispaa ya
Singida ambako yuko kwa ziara ya kikazi mkoani Singida.
Amesema azma ya serikali
inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kuwa
wananchi hususani ambao bado wanaishi katika umaskini wa kipato, kupitia
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanawekewa mazingira yatakayowawezesha
kutumia fursa za Mpango huo kujiletea maendeleo ili hatimaye waweze
kuondokana na umaskini.
“Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John
Pombe Magufuli anayo dhamira ya dhati katika kuboresha maisha ya
wananchi, kinachotakiwa kwenu nyie Walengwa wa TASAF ni kumuunga mkono
kwa kutumia vizuri fursa zilizoko kwenye Mpango huu ulioanzishwa na
Serikali kupitia TASAF” amesisitiza Dkt. Mwanjelwa.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa
rai kwa walengwa wa TASAF kuhakikisha kuwa wanatumia ipasavyo huduma za
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ikiwamo kuwapeleka shule watoto na
kufuatilia mahudhurio yao huku pia akiwataka kuanzisha shughuli za
uzalishaji mali ili kujiongezea kipato.
Naibu Waziri huyo wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pia amezungumzia
sehemu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambayo
inatarajiwa kuanza baada ya kuzinduliwa rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt
Magufuli, kuwa mkazo umewekwa katika kuhakikisha kuwa Walengwa wa Mpango
wenye uwezo wa kufanyakazi wanatumia nguvu zao katika utekelezaji wa
miradi itakayoibuliwa kwenye maeneo yao chini ya utaratibu ujulikanao
kama ajira za muda.
“Serikali inasisitiza kila
mwananchi mwenye uwezo wa kufanyakazi ni lazima atumia uwezo wake huo
katika shughuli za kufanyakazi ili kutoa mchango katika ujenzi wa taifa,
hata hivyo wazee na walengwa ambao hawana uwezo wa kufanyakazi kutokana
na matatizo mbalimbali yakiwemo maradhi ya muda mrefu serikali kupitia
TASAF itaendelea kuwahudumia ” amefafanua Dkt. Mwanjelwa .
Wakitoa ushuhuda wa namna
walivyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini baadhi ya Walengwa
wameishukuru Serikali ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendelea
kuwathamini na kuwarejeshea matumaini kupitia Mpango huo unaotekelezwa
na Serikali kupitia TASAF.
“Tumeweza kuboresha makazi yetu,
kumudu huduma kwa watoto wetu katika sekta ya elimu na afya na kuanzisha
miradi ya ufugaji wa kuku, mbuzi na ng’ombe baada ya kujumuishwa kwenye
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini” amesema mmoja wa Walengwa Bi. Rebeca
Mnyawi mkazi wa eneo la Mtipa nje kidogo ya Manispaa ya Singida.
Mhe.Dkt. mwanjelwa yupo ziarani
Mkoani Singida kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF na
kukutana na Watumishi wa sekta mbalimbali za umma mkoani humo.
Na Happiness Shayo, Singida
Serikali imeweka mkakati wa
kuboresha huduma zinazotolewa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- ili ziweze
kuwanufaisha zaidi Walengwa wa Mpango huo na hatimaye kupunguza umaskini
nchini.

No comments:
Post a Comment