Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akifatilia Uingizwaji wa Taarifa
za Wananchi waliotoka sehemu mbalimbali mkoani Morogoro
na kufika Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),zilizopo
eneo la Tungi-Mfuruni mkoani hapo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la
kujipatia kitambulisho hicho kwa wananchi nchini kote.Wapili kulia ni Afisa Usajili wa NIDA Mkoa wa Morogoro,James Malimo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Afisa Usajili wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Mkoa wa Morogoro,James Malimo(aliyenyoosha
mkono),akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),aliyefika Ofisi ya NIDA zilizopo
eneo la Tungi-Mfuruni kuona zoezi la uandikishaji na utolewaji wa
vitambulisho linavyoendelea.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
********************************
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amepiga marufuku
watu
wanaojiita mawakili na kuwatoza wananchi kiasi cha fedha kinachozidi
shilingi Elfu Kumi wakidai ni ada ya kupewa nyaraka mbadala ya cheti
cha kuzaliwa ikiwa ni hitajio la msingi kwa wananchi wanaofika ofisi
mbalimbali nchini za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)
Akizungumza baada
ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Mkoa wa Morogoro
walioitaka Serikali kuweka bayana kama kupata vitambulisho vya taifa
lazima ulipe hela,Naibu Waziri Masauni alisema vitambulisho hutolewa
bure hakuna haja ya kulipa gharama yoyote huku akipiga marufuku wananchi
kutozwa fedha nje ya ofisi za NIDA
“Kuanzia sasa
kila Ofisi ya NIDA itakuwa na mawakili wa serikali wataohusika na
kuandaa pamoja kuhakiki nyaraka mbalimbali za wananchi wanaokuja kwa
ajili ya vitambulisho vya taifa na ninatoa maelekezo kwa nchi nzima
katika ofisi za NIDA kuwaondoa watu wanaowaandalia wananchi nyaraka hizo
kwanza hatuwatambui kama ni maafisa sheria sahihi au la na wanaweza
kuwathibitisha watu ambao sio raia wakapata vitambulisho kama raia”
alisema Masauni
Akizungumza
katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema wao
kama mkoa wako tayari kuleta mawakili wa serikali katika ofisi hizo za
NIDA huku akiwaasa wananchi kwenda sehemu sahihi wanapofika kutafuta
vitambulisho katika ofisi hizo.
“Serikali ipo
kuhakikisha zoezi la utolewaji namba na vitambulisho vya taifa
linamalizika ndani ya siku 20 zilizoongezwa na Rais Magufuli na kama
mkoa tunayafanyia kazi maelekezo ya Naibu Waziri Masauni na kuanzia
kesho mawakili wa serikali watakuwepo hapa kuhakiki na kutengeneza
nyaraka za serikali kwa wananchi” alisema RC Sanare
Nae Afisa Usajili
wa NIDA Mkoa wa Morogoro,James Malimo amesema katika Mkoa wa Morogoro
na Wilaya zake jumla ya vitambulisho 347,466 kati ya 849,436
vimezalishwa huku maombi 237.236 yakikwama kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo waombaji kukosa vigezo vya uraia,mihuri ya wadau na viambata.
No comments:
Post a Comment