Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi
akizungumza na wafanyakazi wa Wizara yake leo Jijini Dodoma wakati
alipokua akifunga Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ambalo amewakumbusha
watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu na weledi mkubwa kwa maendelo ya
Wizara na taifa kwa
ujumla.
Mkurugenzi
Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Bw.Bernad Patrick akiwasilisha mada kuhusu idara yake katika
Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo lilifanyika kwa siku mbili
januari 30 -31 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Bw.Petro Lyatuu akiwasilisha mada kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2019/2020
na vipaumbele vya bajeti ya 2020/2021 katika Baraza la wafanyakazi wa
wizara hiyo lilifanyika kwa siku mbili januari 30 -31 Jijini Dodoma.
*****************************
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dodoma.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally
Possi amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa
bidiii, uadilifu na kufuata
sheria na kanuni za Utumishi wa Umma ambao ndio muongozo wa utekelezaji
wa majukumu yao ya kila siku katika kuwahudumia wananchi.
Dkt.
Possi ameyasema hayo leo wakati wa kufunga kikao cha Baraza la
Wafanyakazi lililofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma lililokua na
lengo la kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2019/2020 na
kuweka vipaumbele vya bajeti ijayo 2020/2021 pamoja na kujadili namna
bora ya kusukuma mbele gurudumu la Wizara na kuboresha maslah ya
wafanyakazi ili kuongeza tija na kuleta ufanisi katika utendaji wao wa
kazi.
“Baraza
hili limedhamiria kuleta mabadiliko katika Wizara yetu yatakayoleta
matokeo chanya, natoa wito kwa wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa
uadilifu kujituma na kushirikiana ili Wizara yetu ilete maendeleo
yaliyokusudiwa na nchi” alisema Dkt. Possi.
Aidha,
amewataka Wakuu wa Idara kuondoa umbali uliopo kati yao na watumishi
bali washirikiane na wawe wazi kujadili majukumu ya idara kwa upendo na
pia waepushe upendeleo ili Wizara iwe sehemu nzuri ya kufanya kazi kwa uhuru.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa tawi la TUGHE Wizara ya Habari, Utamaduni
Sanaa na Michezo Bw. Mfaume Said amesema kuwa Baraza limekua na manufaa
kwa kuwa hoja
zilizowasilishwa na watumishi zimefafanuliwa vizuri na ambapo anaamini
wafanyakazi watazifanyia kazi kwa weledi zaidi ili kuleta matokeo
yanayokusudiwa.
No comments:
Post a Comment