
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto)
akisikiliza taarifa ya mkoa kutoka kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Dkt. Atupele Mwandiga wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani
Iringa kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani humo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
akisalimiana na kuzungumza na mzee aliyekutana naye akipatiwa huduma
katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku
mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua wodi katika Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani
humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.Faustine Ndugulile akikagua
nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua maabara katika
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili
mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua stoo ya dawa katika
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili
mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
akiangalia mfuko unatumikia kuweka unga lishe unaotengenezwa na Kiwanda
cha Ruaha Milling mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili
mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimpima
mtoto uzito katika siku ya lishe katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa
wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya
na Maendeleo ya Jamii.


Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndugulile akishiriki kupika uji lishe kwa ajili ya watoto katika katika
siku ya lishe katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa wakati wa ziara
yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya
Jamii.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………….
Na Mwandishi Wetu Iringa
Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndugulile amemuagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele
Mwandiga kuhakikisha anapata taarifa ya utoaji wa dawa katika Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Agizo hilo
limekuja mara baada ya ziara ya yake mkoani humo alipotembelea hospitali
hiyo
kujionea utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kushuhudia mmoja
wa mama aliyejifungua Hospitalini hapo kupewa dawa mara moja badala ya
mara tatu kama iilivyoandikwa na Daktari.
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa amekasirishwa na utendaji kazi wa manesi katika
wodi ya Mama na Mtoto kwa kutozingatia utoaji huduma hasa kuhakikisha
wazazi na watoto wanapewa dawa kwa wakati zinazotakiwa na kwa idadi
sahihi.
Ameongeza
kuwa lengo la mgonjwa kupewa huduma ni kuhakikisha anapona na sio
kufanya aendelee kupata tabu na shida hivyo Serikali ya Awamu ya Tano
imewekeza fedha nyingi katika kuhakikisha Sekta ya Afya inaboreshwa
nchini.
“Haiwezekani
mgonjwa kanunua dawa zake kwa fedha zake lakini bado hata hamzingatii
kumpatia dawa mnategemea ataponaje” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt.
Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa
kuhakikisha wanaratibu utoaji wa huduma hospitalini hapo ili kuepukana
na malalamiko ya wagonjwa na kupoteza imani ya wananchi kwa Hospitali
hiyo.
“Tukiendelea
hivi tutaondoa imani kwa wananchi wetu katika utoaji wa huduma za afya
sisi tunatakiwa kutoa huduma kwa wananchi na sio kuwapa kero wananchi”
alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa upande
wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga
amemuahikikishia Naibu Waziri Dkt. Ndugulile kusimamia utoaji huduma
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kusimamia vilivyo ili
kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili.
Ameongeza
kuwa Serikali ya Awamu ya tano imetoa kiasi cha Billioni 7 kwa ajili ya
ujenzi wa Hospitali za Wilaya na maboresho katika Zahanati na vituo vya
Afya mkoani humo katika kuhakikisha inaboresha Sekta ya Afya hivyo
watasimamia Sekta hiyo kikamilifu.
“Mhe. Naibu
Waziri tutahakikisha hatutopoteza imani ya wananchi katika utoaji huduma
za afya na tutatendea haki rasimali fedha tulizopewa na Serikali katika
kuboresha Sekta ya Afya Mkoani kwetu” alisema Dkt. Atupele
Wakati huo
huo Dkt. Ndugulile ametembelea na kujionea utendaji kazi utoaji wa
huduma kwa wananchi katika Ofisi ya Bima ya Afya (NHIF), Kampeni ya
masuala ya Lishe, Kiwanda cha Ruaha Milling na ujenzi wa Hospitali ya
Wilaya ya Kilolo.
Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndugulile yuko katika ziara ya siku mbili mkoani Iringa kukuagua
shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani humo.
No comments:
Post a Comment