Pages

Wednesday, January 1, 2020

DK.SHEIN AWATUNUKU WAHITIMU WA MAHAFALI YA 15 CHUO CHA TAIFA ZANZIBAR SUZA TUNGUU



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwatunuku Wahitimu Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( SUZA) wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo hicho yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein (SUZA) Tunguu Wilaya ya Kati Unguja (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe.Riziki Pembe Juma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Prof. Joyce Ndalichako
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuki Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili Bi. Mwanahija Ali Juma, wakati wa Mahafali ya 15 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubiwa wakati wa hafla ya Mahafali ya 15 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora wa Kike Ngazi ya Shahada ya Kwanza ya Jiografia na Taaluma ya Mazingira. Aisha Omar Makame.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment