Diamond Platnamz akiongea kwa
simu na Rais Dkt John Pomre Magufuli wakati alipompigia akiwa katika
onesho lake la miaka 10 lililofanyika kwenye uwanja wa Tanganyika mjini
Kigoma kushoto ni Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM
Taifa na kulia ni Babu Tale Meneja wake.
***********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
hapa nchini Naseeb Abdul maalufu Diamond Platinumz usiku wa kuamkia leo
alikuwa akitumbuiza katika kwenye uwanja wa Tanganyika mjini
Kigoma
kusherekea miaka 10 tangu aanze muziki wa Bongo Fleva.
Akiwa jukwaani Diamond Platnumz
aliletewa simu na Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa
CCM iliyopigwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John
Pombe Magufuli ili kuzungumza naye, Rais Magufuli alimpongeza Diamond
kwa jitihada zake anazofanya katika sanaa katika kulitangaza Taifa kwa
ujumla na kusaidia vijana wenzake.
Rais Magufuli alianza kwa
kumpongeza Diamond nakusema weweni mwanaume unafanya kazi nzuri na mimi
nakupenda sana na natambua kazi yako nzuri unayoifanya.
Kupitia simu hiyo Rais Magufuli
aliuambia umati mkubwa uliokuwa umekusanyika katika tamasha hilo kwamba
atahakikisha barabara ya Kigoma Mpaka Nyakanazi inakamilika kwa kiwango
cha lami katika maeneo ambayo bado hayajakamilika ili wananchi wa
Kigoma wasafiri bila usumbufu.
Naye Diamond hakuchelewa kutupa ombi lake akimtaka Rais kuwasaidia wasanii wa Tanzania.
“Asante sana nimekusikia,”
alisema Rais Magufuli. “Lakini nakupongeza sana kwa kuzidi kuitangaza
Tanzania katika masuala ya muziki na nawapongeza wanamuziki wote hata
wale wanaoigiza nawapenda sana asanteni jamani.” Alisema Mh. Rais
Magufuli.
No comments:
Post a Comment