
Na Silvia Mchuruza.Bukoba.
KUTOKANA na ongozeko la abiria wa usafiri wa anga mkoani Kagera,
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limeongeza ndege ya pili ili
kukabiliana na kiwango cha abiria mkoani humo.
Mtendaji Mkuu wa
ATCL, Mhadisi Ladisraus Matindi amesema kuwa Mkoa wa Kagera una zaidi ya
abiria 2,400 kila mwezi sawa na asilimia 70 za ujazo wa ndege kwenda na
kurudi
Matindi ameyasema hayo leo mkoani Kagera alipofanya ziara ya
kawaida ya kikazi kwa ajili ya kuongea na wadau wa shirika hilo na
kuongeza kuwa katika kipindi cha msimu wa sikukuu, ATCL imelazimika
kuleta ndege mbili ili kumudu wingi wa abiria.
Amesema licha ya kuongeza ndege ya pili ambapo
zote zinafanya kazi kila siku lakini kwa mujibu wa Meneja wa uwanja wa
ndege wa Bukoba, ni kwamba ndege zote zimejaa hadi Januari 15.
Pia Matindi ametolea ufafanuzi wa malalamiko
ambayo yamekuwepo kwa abiria wa usafiri huo kuhusu mizigo yao kukwama
uwanja wa ndege kuwa na changamoto hiyo inatokana na uwanja wa ndege wa
Bukoba kuwa mfupi.
Matindi alisema changamoto ya uwanja huo wa ndege inaendelea kutatuliwa ili ziweze kutua ndege kubwa
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali
Marco Gaguti amewaomba wakazi wa Mkoa wa Kagera kutumia usafiri wa anga
kiuchumi zaidi ili kukuza uchumi wa nchi na mkoa na hata kwa wananchi
wenyewe kutokana na kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo zinaweza
kusafirishwa nje ya mkoa pia.
“Tumeshaanza hatua za awali za kupanua uwanja
huo na kutokana na mahitajio ya wateja Mkoa utaweka msukumo ili upanuzi
uende kwa haraka ambapo upanuzi huo utaenda sambamba na kuweka taa ili
kusaidia ndege kutua wakati wa mawingu na usiku” alisema Gaguti.
No comments:
Post a Comment