Na Mwandishi Maalum – Mwananyamala
Watanzania hususan wakazi wa jiji
la Dar es Salaam, wametakiwa kuhakikisha wanazingatia na kufuata mfumo
wa rufaa wa utoaji huduma za afya nchini uliowekwa na Serikali.
Rai hiyo imetolewa leo na
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Akiwa hospitalini hapo, Waziri
Ummy alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliowasindikiza ndugu zao
kwenda kujifungua, kwamba wanalazimishwa kulipia gharama ingawa Sera ya
Serikali inaeleza huduma ya kujifungua ni bila malipo.
Hata hivyo, ilibainika kwamba
idadi kubwa ya wajawazito wanaofika hospitalini hapo kujifungua
hawafuati mfumo wa rufaa badala yake huenda wenyewe hospitalini hapo.
Kutokana na hali hiyo, wananchi hutakiwa kuchangia huduma ingawa wengi wao walilalamika kwamba hawapewi maelezo ya kina hasa kuhusu huduma ya kujifungua kwa haraka (fast track) iliyoanzishwa hospitalini hapo.
Kutokana na hali hiyo, wananchi hutakiwa kuchangia huduma ingawa wengi wao walilalamika kwamba hawapewi maelezo ya kina hasa kuhusu huduma ya kujifungua kwa haraka (fast track) iliyoanzishwa hospitalini hapo.
“Kwa kutokufuata rufaa ndiyo maana
kunakuwa na mrundikano wa wagonjwa. Taarifa za madaktari zinaeleza
wajawazito 85 kati ya 100 wanaweza kujifungua bila changamoto yoyote na
wanaweza hata kuzalishwa na wakungwa wa ngazi ya cheti au diploma.
“Ni asilimia 15 hupata changamoto
za uzazi na hao ndiyo wanaopaswa kupewa rufaa kwa mfano waje huku
Mwananyamala,” amesema Waziri Ummy.
Ameongeza “Hivyo, nimewaeleza wazi
uongozi kwa hawa wanaokuja bila rufaa wasione aibu kuwapiga penati,
lakini wale wanaokuja kwa kufuata mfumo wa rufaa wapewe huduma bila
malipo inavyostahili.
Sambamba na hilo, ameuagiza
uongozi huo kuhakikisha unaweka uwiano sawa wa madaktari katika upande
wa huduma hiyo ya fast track waliyoainzisha na isiwe kichocheo au
kisababishi cha watu kukosa huduma.
“Hii itawezesha hospitali
kujiendesha ili itoe huduma bora, wameweka kiasi cha Sh. 75,000 badala
ya Sh. mil 1.5 ambazo wanalipia kule hospitali binafsi, muhimu kutoa
maelezo sahihi kwa wananchi,” amesema.
Awali, Mganga Mfawidhi wa
Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu amesema walianzisha huduma hiyo ya fast
track ili kuwezesha wananchi wenye kipato cha chini wanaohitaji huduma
ya haraka kujifungua nao waweze kuimudu.
“Watu wanakuja hapa Mwananyamala
kwa sababu ya huduma zetu ni bora, zaidi ya asilimia 90 tunaowahudumia
ni wanawake na watoto na asilimia 15 pekee huhitaji huduma ya dharura
kujifungua.
“Hapa tuna madaktari bingwa 22,
tulianzisha huduma hii ili hawa mabingwa waweze kutoa huduma hapa hapa
badala ya kwenda kule hospitali binafsi, lakini hakuna mwananchi ambaye
hatukumpa huduma na kumlazimisha alipie kwanza gharama,” amesema.
Ameongeza “Hatulazimishi mwananchi
kulipia huduma, tunatoa huduma kwa wote, lakini ukichagua kuja
Mwananyamala badala ya sisi kukurudisha tunakuambia kuna njia mbili,
upate huduma kwa ‘fast track’ au ufuate mfumo wa rufaa.
No comments:
Post a Comment