
Na.Ashura Mohamed -Arusha.
Wachimbaji,madalali
na wafanyabiashara wa Madini Mkoa wa Arusha wamemwaomba Waziri Wa
Madini Dotto Biteko leseni za Kanda zitumike nzima ili kuuza Madini ya
aina mbalimbali Kwa Mataifa mengine.
Wameyasema hayo
katika mkutano wa wadau wa Madini uliohudhuriwa na
wafanyabiashara,madalali na wachimbaji pamoja na vyama vya wachimbaji
mmoja wa wachimbaji hao Samweli Rugamalira Amesema nitakribani miaka 8
tangu aanze kazi hiyo ya uchimbaji Madini aina ya Tanzanite ,ameiomba
wizara kuangalia namna ya kuziboresha na ziweze kutumia Nchi nzima.
Alieleza changamoto
ya ajira ndani ya machimbo ya mererani jambo ambalo limeibua mjadala
kwa wafanyabiashara wanaochimba madini kuwa ni lazima walipie shilingi
milioni 400 hadi 500 jambo ambalo limeonekana kuleta utata, nakumowmba
waziri biteko kuingilia kati .
kwa Upande wa
madalali akiwemo Tupilike Samson Mwangosi aliiomba Wizara kuwatambua
na kuwapatia ofisi ili kuweza kutekeleza kazi zao mana wamekuwa
wakifanyabiashara kwa njia ya mali kauli jambo ambalo linafifisha
utendaji wao nakuiomba Tume na wizara kusaidia.
Mwenyekiti wa chama
cha wafanyabiashara wa Madini Tanzania(Tamida) Sammy Mollely alisema
wapo tayari kuongeza thamani ya Madini nchini lakini bado
kunachangamoto ya ya vikwazo vya vibali kwa wataalamu wa
usanifu,ungarishaji,na uwekaji wa Urembo(nakshi) kuchukuwa muda Mrefu
pindi wanapoomba uku matarajio yao nikupata wataalamu kutoka nchi ya
Srilanka ili kuongeza Ujuzi.
Sammy alisema kuwa
uwepo wa Tasac imekuwa kikwazo kikubwa na kueleza na kero kwao hali
inayochangia kudidimiza uchumi wa nchi,kwani uchukuwa Miezi 2 kupata
kibali kusafirisha madini nakueleza ikiwezekana Tasac Ingeondolewa
kwani haina msaada kwao.
Naye Mbunge wa
Simanjiro James Olemilya alisema wilaya hiyo ndiyo kitovu cha
uchimbaji wa madini lakini bei ya Madini ya Tanzanite imeonekana
kuyumba nakuiomba wizara kufanyika uchunguzi wa kina nakubahini
kilichojificha ili kuwabahini watu wanaochezea bei ya Tanzanite na
kutokuipatia Nchi Hasara ..
Waziri wa Madini Mh
Dotto Biteko amesema wafanyabiashara wa sekta ya Madini wanayo
changamoto yakuifata njia isiyosahihi nakujikuta wanatoka nje ya
Mstarikibiashara ,jambo ambalo amesisitiza kufuata hatua zaki sheria
kwani sekta hiyo haiwezi kusimamiwa na Waziri mwenyewe uku serikali
ikitaka uwazi wakibiashara na kuhitaji fedha ili kuweza kutekeleza
Huduma zakijamii .
Biteko ameongeza kuwa
Mheshimwa Rais Wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Maguguli
Anandoto kubwa yakuifikisha Nchi katika Uchumi wakati na anachukizwa na
mfanyabiashara anayetorosha Madini na kukwepa kodi ,na kusissitiza
serikali inataka kuvutia wageni kuja kununua Madini kwa haki Nchini.
Naibu Waziri wa
Nchi,ofisi ya Waziri mkuu, Sera,bunge kazi, Vijana,na wenye Ulemavu Mh
Antony mavunde Amesema nchi inawahitaji wataalamu wa Madini kwa Asilimia
kubwa kutoka Nchi ya Kenya na Srilanka ,nakuanzia mwakani Wizara yake
itaanza kuliwekea mikakati katika uratibu wa wa vibali vya kazi kwa
Wageni ,nakueleza kuwa katika kutatua changamoto ya vibali Vya kazi
wizara imekuja na Mfumo mtandao wakupata Kibali cha kazi ili kuondoa
urasimu nakupiga marufuku kwa watu wa kati kama waleta maombi,
nakuwataka wafanyabiashara kupeleka wenyewe maombi yao.
Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Steven Zelothe amepongeza utaratibu
huo wa Mkoa kukutana na wadau wa Madini kusikiliza kujadili na
kutatua changamoto zao na kuongeza wigo mpana wakibiashara ndani na nje
ya Nchi nakusisitiza chama kitaendelea kuunga mkono serikali na
kutekeleza ilani ya ccm ikiwemo wachimbaji kunufaika na sekta hiyo
katika kuongeza mapato kwani ndiyo dhamira kuu ya serikali kua na
soko kubwa la Madini kimataifa duniani.
No comments:
Post a Comment