Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan
nchini Tanzania, Bw. Katsutoshi Takeda, wakisaini mkataba wa Msaada wa
Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan
nchini Tanzania, Bw. Katsutoshi Takeda, wakibadilishana mkataba wa
Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania
(TAFICO) ambapo TAFICO itaweza itaweza kuwa na Meli ya Uvuvi, hafla hiyo
iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan
nchini Tanzania, Bw. Katsutoshi Takeda, wakiwa wamenyenyua Mkataba wa
Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania
(TAFICO), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na
Maafisa waandamizi (mbele) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara
ya Mifugo na Uvuvi, wakishuhudia kusainiwa kwa mkataba wa Msaada wa Sh.
4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (katikati) akieleza kuhusu misaada na mikopo
yenye masharti nafuu inayotolewa na Japan, wakati wa hafla ya kusainiwa
kwa Mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi
Tanzania (TAFICO), Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Balozi wa
Japan nchini Tanzania, Bw. Katsutoshi Takeda na kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa upande wa Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, kwa upande wa Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, akielezea jitihada za
Serikali za kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia), na Kaimu
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Katsutoshi Takeda (wa tatu kulia)
wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Japani baada
ya hafla ya kusainiwa kwa mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya
kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)
……………..
Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Tanzania imepokea
msaada wa Yen za Japan milioni 200 sawa na Shilingi Bilioni 4.2 kutoka
Serikali ya Japan kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania
(TAFICO)
Mkataba wa
msaada huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Doto James, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu na Kaimu Balozi
wa Japan, Bw. Katsutoshi Takeda, kwa niaba ya Serikali ya Japan.
Katibu Mkuu,
Bw. Doto James, alisema kuwa msaada huo utatumika kununua Meli ya Uvuvi
yenye vifaa vya kisasa, mashine ya kutengeneza barafu, ghala la baridi
la kuhifadhia samaki, Vifaa mbalimbali vya kuvulia samaki na vya
karakana, gari lenye mitambo maalum ya barafu na Gari kwa ajili ya
kusambazia samaki.
Alisema
kuwa utekelezaji wa Mradi huu utachangia kwa kiasi kikubwa katika
kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Awamu ya Pili
(FYDP II), ambayo pamoja na mengine unalenga kuboresha Sekta ya Uvuvi na
hatimaye kuvutia Watanzania zaidi kujihusisha katika Sekta ya Uvuvi
kama shughuli kuu ya kujipatia kipato.
“Mradi huu
utaongeza uuzaji wa samaki nje ya nchi, kuongeza uhakika wa chakula
nchini, na pia utaboresha usindikaji wa samaki, kuongeza thamani na
masoko na kupunguza upotevu wa mazao ya samaki baada ya kuvua”, alieleza
Bw. James.
Alisema
kuwa Kiwango cha ukuaji kwa shughuli ndogo za kiuchumi za uvuvi
kilifikia asilimia 9.2 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia
8.4 mwaka 2017 ambapo kiwango kikubwa cha ukuaji kilitokana na utunzaji
mzuri wa mazalia ya samaki yakiwemo mabwawa ya watu binafsi sambamba na
kuongezeka kwa mahitaji katika soko la ndani na nje.
Bw. James
alisema kuwa, shughuli za uvuvi zilichangia asilimia 1.7 katika Pato la
Taifa mwaka 2018, ambayo inadhihirisha umuhimu wa uvuvi katika uchumi,
hivyo msaada uliotolewa utachangia jitihada za Serikali katika kufikia
Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, Malengo Endelevu ya mwaka 2030 na
Agenda ya Maendeleo ya Afrika ya mwaka 2063.
Alisema kuwa
Serikali ya Japan imekuwa ikiisaidia Tanzania kupitia misaada na mikopo
nafuu katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Miundombinu ya barabara,
Maji, Nishati Utawala Bora na Uwajibikaji ambapo mpaka sasa Jumla ya Sh.
Trilioni 1. 3 zimetolewa na Serikali hiyo tangu mwaka 2012.
Misaada na
mikopo hiyo inadhihirisha kuwa kuna uhusiano mzuri wa kirafiki kati ya
Tanzania na Serikali ya Japan, hivyo matumaini ni kuwa urafiki huo
utaendelea kuimarishwa na Serikali zote mbili kwa ajili ya maendeleo ya
nchi hizo.
Kwa upande
wake Naibu na Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Katsutoshi Takeda, kwa niaba ya
Serikali ya Japan amesema nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania
kutokana na ushirikiano mzuri kati ya nchi hizo mbili lakini pia
kuchangia jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi na
kuondoa umasikini wa wananchi wake.
Naye Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamahtamah ameishukuru
Serikali ya Japan kwa msaada huo utakaosaidia kufufua Shirika hilo la
Uvuvi.
Alisema kuwa
Serikali itapeleka mswaada Bungeni mwezi Januari mwakani, ili
kuliwezesha TAFICO kuanza kazi zake rasmi na kwa kishindo ili Shirika
hilo liweze kuchangia katika uchumi wa Taifa kwa kiwango kikubwa.
Alisema kuwa
pamoja na msaada huo, Serikali imechukua hatua za kuchambua mali
zilizokuwa zikimilikiwa kinyemela na baadhi ya taasisi na watu ambapo
mpaka sasa mali zenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 118 zimerejeshwa
Serikalini na kazi ya kurejesha mali nyingine zinaendelea kwa
kushirikiana na Msajili wa Hazina.
No comments:
Post a Comment