N/Waziri wa Viwanda na
Biashara Eng. Stellah Manyanya (wa pili Kushoto) akitoa maelekezo kwa
Msajili wa Bodi ya Usajili Wataalamu wa Miapango Miji nchini Hellen
Mtutwa (Kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika Mkutano
wa Wataalamu wa Mipango mwishoni mwa wiki.
N/Waziri wa Viwanda na
Biashara Eng. Stellah Manyanya (katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili
wa Wataalamu wa Mipango Miji Profesa Wilbert Kombe (Kushoto) na Msajili
wa Bodi ya Wataalamu wa Mipango Miji Hellen Mtutwa ( kulia) wakiwasili
katika Mkutano wa Wataalamu wa Mipango Miji Nchini uliofanyika jijini
Dodoma mwishoni mwa wiki.
N/Waziri wa Viwanda na
Biashara Eng. Stellah Manyanya (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Wataalamu wa Mipango Miji na baadhi ya wajumbe
kwenye Mkutano wa Wataalamu wa Mipango Miji Nchini uliofanyika
Mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
………………..
Na Munir Shemweta, WANMM DODODMA
Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya ametaka kushirikishwa kwa
sekta ya ardhi hasa idara ya Mipango Miji katika miradi mbalimbali
inayoibuniwa na serikali ili
kuondokana na miradi isiyokuwa na tija kwa
jamii.
Mhandisi Stellah
Manyanya aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano mkuu wa sita
wa Mwaka wa Wataalaamu wa Mipangomiji uliofanyika jijini Dodoma.
Alisema, kumekuwepo
na miradi mingi nchini inayoanzishwa na Serikali na kutumia gharama
kubwa lakini matokeo yake imekuwa haitumiki ipasavyo na wakati mwingine
inaingiliana na shughuli nyingine za kijamii hali inayosababisha kuzuka
kwa migogoro kwenye jamii.
Alitolea mfano Jengo
la Machinga Complex lililopo Ilala Jijini Dar es Salaam, Mhandisi
Manyanya alisema, kutokuwepo kwa mipango kina ya muda mrefu na utafiti
duni ndio chanzo kikubwa hadi leo jengo hilo limeshindwa kufikia lengo
walilojiwekea la kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo katika shughuli
zao.
“ Kuna wale wenzetu
waliojenga lile Jengo kubwa kabisa wakalipa jina la heshema Machinga
Complex lakini kwa namna walivyopanga na kutumia fedha kwenye kujenga
limebaki kuwa jengo la aibu” Alisema Mhandisi Stellah Manyanya.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Wilbert Kombe alisema, Miradi Mingi
nchini inafanyika bila kushirikisha wataalamu wa Mipangomiji kwani
Taasisi nyingi za Serikali zinapopanga mipango yake ya kiuchumi na
miundombinu hazizingatii na kuonesha mipango ya ardhi hali
inayosababisha muingiliano wa shughuli za kiuchumi.
Aliongeza kwa kusema
kuwa, Taasisi zote nchini zinategemea uwepo wa ardhi, hivyo hazina budi
kushirikiana na Sekta zote zinazohusu ardhi kabla ya kupanga mipango yao
ya kiuchumi ili kuepusha muingiliano na kupangwa vibaya kwa miji.
‘’Ukitazama eneo la
Maegesho ya magari ya Mwendokasi eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam ,
hayo ni matokeo ya kutoshirikishana katika mipango miji kwani lilile
eneo linahitaji mambo mawili ama lihamishwe au iinuliwe barabara kuanzia
Magomeni “ Alisema Profesa Kombe.
Naye Msajili wa Bodi
ya Wataalamu wa Mipango Miji Hellen Mtutwa alisema, taasisi zote za
Serikali ni lazima ziwe na ushirikiano wa karibu wakati wa kuandaa
mipango na kuitekeleza siyo sekta za ardhi tu bali Tanesco ,Tanroad
Maji na taasisi nyingine ili kuepusha hasara kwa Serikali .
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed alisema,
maendeleo yote yapo kwenye sekta ya ardhi hivyo Serikali inatakiwa iipe
kipaumbele sekta hiyo kwani hasara ya kutokufanya mipango ni kubwa
kuliko kuitekeleza.
No comments:
Post a Comment