Pages

Sunday, December 29, 2019

MWILI WA FARU FAUSTA KUKAUSHWA



******************************
Faru mkongwe duniani anayekadiriwa kuwa na umri mkubwa kuliko faru wote duniani anayejulikana kwa jina la Fausta ambaye amekufa hivi karibuni anatarajiwa kukaushwa na
kuhifadhiwa kwenye jumba la la Makumbusho Ngorongoro.

Ameyaema hayo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangala baada ya kutokea kifo cha Faru huyo ambaye alikuwa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

“Tunakusudia kumkausha na kuutunza mwili wake kwenye Jumba la Makumbusho pale eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, aidha ninawapongeza sana wahifadhi wetu wa Ngorongoro kwa kazi nzuri ya kumtunza Faru Fausta, Faru wengine wengi na Hifadhi yote kwa ujumla”. Amesema Dkt.Kigwangala.

Faru Fausta amekufa akiwa katika banda maalumu alilokuwa amehifadhiwa kwa zaidi ya miaka mitatu kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

No comments:

Post a Comment