Pages

Sunday, December 29, 2019

BALOZI WA TANAPA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MKOMAZI,AHIMIZA WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA




BALOZI wa Tanapa nchini Nancy Sumari kushoto akizungumza wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na kuzinduliwa na Mkuu
wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule kulia kuhusu umuhimu wa watanzania kutembelea vivutio vya utalii
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa uzinduzi  wa  kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
MKUU  wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel
Mtui kushoto akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo  katikati ni Balozi wa Tanapa Nancy Sumari na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni
ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kushoto ni Balozi
wa Tanapa Nancy Sumari na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui kushoto

Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini uliofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kushoto ni Balozi wa Tanapa Nancy Sumari na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui
Balozi wa Tanapa nchini  Nancy Sumari katikati akiwa ameshika kikombe akiwa na Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule kulia na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui kushoto wakati wa uzinduzi huo
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule kulia akipongezana na Balozi wa Tanapa nchini Nancy Sumari kushoto mara baada ya kufanya uzinduzi huo kushoto ni Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui
Balozi wa Tanapa nchini Nancy Sumari katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abeli Mtui kushoto wakati wa watalii wa ndani waliotembelea hifadhi hiyo wakati wa uzinduzi huo
Muongoza watalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kulia akitoa maelezo mafupi kwa Balozi wa Tanapa nchini Nancy Sumary wakati aliptembelea hifadhi hiyo
 BALOZI wa Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Nancy Sumari katika akiwa na baadhi ya watalii wengine wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani
Sehemu ya msururu wa magari ukiwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
BALOZI wa Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Nancy Sumari ametembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro huku akiwahimiza watanzania kujenga
mazoea ya kutembelea
hifadhi zilizopo hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio vilivyopo na kujifunza
mambo mbalimbali ya uhifadhi wa wanyama pori.


Nancy ambaye aliwahi kuwa Miss Tanzania 2005 na mrembo wa Dunia Afrika mwaka huo aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya kutangaza utalii wa ndani hapa
nchini iliyofanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na kuzinduliwa na Mkuu
wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule.
Alisema kwamba utalii wa ndani ni jambo muhimu sana kwa watanzania kwani unamuwezesha kutumia muda mchache kuweza kujifunza na kujionea vivutio vilivyopo ndani ya nchi na kuweza kuvifurahia.
“Kwa kweli niwashukuru wananchi, Mkuu wa wilaya ya Same na Mhifadhi wa Hifadhi ya
Taifa ya Mkomazi kwa kutukaribisha mimi na familia yangu kutembelea na
kufurahia utalii wa ndani ni jambo nzuri na la kipekee sana  hivyo niendelee kuwasihi watanzania tutembelee hifadhi zetu”Alisema.
Hata hivyo aliwakaribisha marafiki na watanzania wengine kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kwani ni eneo ambalo la kipekee kutokana na kusheheni idadi kubwa ya
wanyama wakubwa na ndege ambao wageni wanakutana nao wakati tu wanapoingia
kwenye eneo la lango la geti hilo.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Abel Mtui alisema kwamba katika kampeni hiyo wageni ambao walijiandikisha kuingia
ndani ya hifadhi ni 78 ambao kati yao kutoka wilaya ya Mwanga ni 13, Same ni 55
na Hedaru ni 10 hivyo hiyo ni idadi kubwa ya kutosha na wanategemea waliokuja
watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.
Alisema anaimani idadi kubwa ya watalii wa ndani itazidi kuongezeka zaidi kwani wageni
waliotembelea hifadhi hiyo wataenda kuwaarifu wenzao huku wageni ambao walipata
fursa ya kutembelea hifadhi hiyo wakipiga picha na Balozi Nancy.
“Hivyo niendelee kuwahimiza watanzania kuendelea kutembelea vivutio vya utalii ambao vipo hapa nchini ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ambayo inavuvutio vya kipekee”Alisema.
Awali akizungumza wakati wa kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule
alkiwakaribisha Balozi huyo na familia yake na wananchi ambao tayari walianza
kujitokeza kwenye kufanya utalii wa ndani kwani wana matarajio makubwa sana na
hifadhi ya mkomazi kutokana na kuwa na vuvutio vingi vinavyopatikana na vya
kipelee ambavyo havipatikana maeneo mengine.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wanatagemea hifadhi ya Taifa ya mkomozi inayokuwa kwa haraka kwa kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ikiwemo kuongeza mapato na kukuza uchumi wa serikali na mwananchi mmoja mmoja.
“Tunaweka nguvu nyingi kama serikali kuhakikisha mkomazi inakuwa na kupata miundombinu na vitu vyengine vitakavyofanya watalii kuvutiw lakini pia ujio wa faru ni kuvutio ambacho kitakuwa hakuna eneo jengine Tanzania hadi ya mkomazi kunajengwa ukuta ambao faru watawekwa pale na upo kwenye hatua zxa mwisho za ukamilishaji”Alisema.
“Kukamilika kwake utawawezesha watanzania ambao watakuwa wakifika Mkomazi anakuwa na uhakika
wa kuona faru na itakuwa hifadhi pekee kwenye nchi ya Tanzania na nchi chache
za Afrika na wanategemea jambo hilo litasaidia kupata idadi kubwa ya wageni “Alisema
Dc huyo.

No comments:

Post a Comment