Pages

Saturday, November 2, 2019

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA BANDA LA TPDC KWENYE MAONESHO YA BIASHARA NA UWEKEZAAJI MKOANI MTWARA


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (mwenye tai ya mistari), akiangalia "ramani" ya jinsi gesi asilia inavyovunwa, kuchakatwa, kutunzwa na kusafirishwa kwa watumiaji, wakati alipotembela banda la Shirika la Manedeleo ya Petroli nchini (TPDC), kwenye maonesho ya biashara na uwekezaji katika viwanja vya chou cha ualimu Mtwara Novemba 1, 2019. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dkt. James Matarajio, wakwanza kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa na wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki  (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), James Mataragio (wa tatu kushoto) kuhusu mtandao visama vya gesi vya Songosongo na Mtwara pamoja na mtandao wa usambazaji na matumizi wa gesi hiyo. Alikuwa akikagua Maonesho ya Biashara Mtwara kabla ya kufungua Mwongozo wa Uwekezaji  wa Mkoa huo,  Novemba 1, 2019. Wa nne kushoto ni Waziri wa Biashara na Viwanda, Innocent Bashungwa
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia kongamano la biashara na uwekezaji mkoani Mtwara
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dkt. James Matarajio akihutubia kongamano la biashara na uwekezaji mkoani Mtwara
Mtaalamu wa Miamba, wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Lucas Luhaga (kushoto), akiwapatia maelezo Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii Nchini (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi.Christine Musisi kuhusu namna gesi asilia inavyozalishwa, kuchakatwa na kusafirishwa kutoka kwenye chanzo hadi kwa watumiaji wakati wa maonesho ya Biashara na Uwekezaji kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu .

Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Dkt. James Matarajio (wapili kulia), akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni tanzu ya TPDC ya GASCO Mhandisi Baltazar Mrosso (wapili kulia), Afisa Mkuu wa Fedha kiwanda cha saruji Dangote Bw.Host Mapondera na Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC, Bi. Marie Mselemu kwenye banda la TPDC wakati maonesho ya biashara na uwekezaji kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara

Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Dkt. James Matarajio (kulia), akiteta jambo na Afisa Mkuu wa Fedha kiwanda cha saruji Dangote kilichoko Mkoani Mtwara Bw.Host Mapondera wakati afisa huyo alipotembelea banda la TPDC kwenye maonesho ya biashara na uwekezaji kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kwenye maonesho ya biashara na uwekezaji mkoani Mtwara yaliyokwenda sambamba na kongamano lililowaleta pamoja wawekezaji na uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji mkoani humo kwenye viwanja vya chuo cha Ualimu Mtwara.
Waziri Mkuu alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Dkt. James Matarajio ambaye alimpa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazotekelezawa na Shirika hilo ikiwa ni pamoja na shughuli za maendeleo ya utafiti na utafiti wa mafuta na gesi na uzalishaji, biashara ya mafuta na gesi  na mipango na uwekezaji.
TPDC inashiriki maonesho hayo ambayo ni sehemu ya kongamano la uwekezaji mkoani Mtwara lililokwenda sambamba na uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji mkoani Mtwara (MIG) ambapo wawekezaji wa ndani na nje walihudhuria na kupata nafasi ya kusikiliza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana mkoani humo ambapo TPDC ilitumia fursa hiyo kuwahakikishia wawekezaji kuwa gesi ya kutosha inapatikana.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Waziri Mkuu aliwahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kufika mkoani Mtwara ili kuwekeza katika maeneo mbalimbali kama vile kilimo, uvuvi, ufugaji, ujenzi wa miundombinu na kubwa zaidi viwanda kwani kuna gesi ya kutosha inayopatikana mkoani humo.
Miongoni mwa wateja wakubwa wa TPDC wanaonunua gesi ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO na kiwanda cha sarufi cha Dangote kilichoko Mkoani Mtwara

No comments:

Post a Comment