Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mgahama, akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Andrew Massawe
na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba, wakati wa kukagua Mradi wa ujenzi wa Kiwanda
cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mkoani Kilimanjaro, Utekelezaji wa
Mradi wa huo unatekelezwa na Mfuko wa PSSSF
na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani
Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mgahama, akipata ufafanuzi kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Magereza, juu
ya ramani ya Kiwanda cha bidhaa za ngozi
cha Karanga, wakati wa kukagua utekelezaji
wa Mradi wa huo unatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia wataalamu
wake wa ndani, leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mgahama, akipata maelezo kutoka Meneja Miradi, PSSF juu ya Mpango kazi
wa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa
Viwanda vya ngozi Karanga unoatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia
wataalamu wake wa ndani, wakati wa kukagua mradi huo leo tarehe 29 Novemba 2019,
mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mgahama, akipata ufafanuzi kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Magereza, juu
ya ramani ya Kiwanda cha bidhaa za ngozi
cha Karanga, wakati wa kukagua utekelezaji
wa Mradi huo unoatekelezwa na Mfuko wa PSSSF
na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani, leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani
Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mgahama, akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Andrew Massawe
na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba mara baada ya kukagua Mradi wa
ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mkoani Kilimanjaro,
Utekelezaji wa Mradi huo unatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia
wataalamu wake wa ndani leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mgahama, amempa miezi miwili mkandarasi anayejenga Kiwanda cha bidhaa
za ngozi cha Karanga, kilichopo mkoani Kilimanjaro, kukamilisha hatua ya kwanza
ya ujenzi wa kiwanda hicho hadi kufikia
tarehe 20 Januari mwaka 2020, ili ujenzi hatua ya pili ya ujenzi wa kiwanda hicho uweze
kuanza mara moja kwa ajili ya kuhakikisha kiwanda kinaanza uzalishaji wa bidhaa
za ngozi.
Mkandarasi huyo
ambaye ni Kikosi cha ujenzi cha Shirika la Uzalishaji la Magereza ameelekezwa
kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ndani ya kipindi hicho kuhakikisha
amejenga majengo manne, ikiwa ni jengo la kuzalisha bidhaa za ngozi na soli za
viatu, jengo la mitambo ya umeme pamoja na ghala la vifaa vya ngozi.
Waziri Mhagama ametoa
maelekezo hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho leo
tarehe 29 Novemba, 2019, mkoani Kilimanjaro, ambapo amefafanua kuwa kiwanda hicho ni muhimu kujengwa kwa haraka
sana kwani kitaiwezesha Tanzania kuufikia uchumi wa viwanda kwa kuwa bidhaa
zitakazozalishwa na kiwanda hicho zina soko kubwa ndani na nje ya nchi hususani
katika Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
“Sisi katika Afrika
ni matajiri wa mifugo na bidhaa zinazolishwa na mifugo, lakini hapa nchini hatuna kiwanda tunachoweza kutegemea katika
bidhaa za ngozi, hivyo ni muhimu kuharakisha ujenzi wa kiwanda hiki ili tuweze
kutengeneza ajira hapa kati ya elfu tatu hadi elfu nne na ukizingatia nguvu
kazi ya nchi yetu asilimia 56 ni vijana.Kiwanda hiki kitakuwa muhimu sana kwa
ustawi wa nchi” Amesema Mhagama.
Mhe. Mhagama amewataka
watekelezaji wa Mradi huo kuhakikisha
wanakuwa na mpango kazi wa kukamilisha kazi hiyo na kuuwasilisha kwake, lakini
pia kuwa na mpango mkakati wa biashara utakao
wezesha kusaidia kupatikana na masoko ya bidhaa hizo. Ameongeza kuwa atakuwa na
watu wakufuatilia kwa karibu shughuli za ujenzi huo ili kuhakikisha ujenzi
unakamilika kwa wakati. Huku akisisitiza Changamoto zozote za utekelezaji wa
Mradi huo zizingatiwe ili pindi ukikamilika zisije anza kuibuliwa na kuweza kukukosesha
mradi kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Ajira, vijana na Watu wenye Ulemavu),
Andrew Massawe, amemuhakikishia Mhe. Waziri Mhagma kuwa, atafuatilia ushughuli
za ujenzi wa mradi huo kwa karibu ili
kuhakikisha maelekezo yake yanatekelezwa kwa kila hatua za ujenzi ili kuhakikisha ujenzi
unakamilika kwa muda uliopangwa.
Naye, Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Hosea Kashimba
amemhakikishia Mhe.Waziri Mhagama kuwa atahakiksha kuwa ujenzi huo unakuwa na
ubora na unakamilika ndani ya muda aliouelekeza ili watanzania waweze kunufaika
na bidhaa za kiwanda hicho lakini pia
waweze kupata ajira za uhakika kutoka
katika kiwanda hicho.
Utekelezaji wa Mradi
wa Ujenzi wa Viwanda vya ngozi Karanga unatekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani
na timu ya washauri elekezi wa viwanda TRIDO.
Mradi wa ujenzi wa
Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga unatokana na Kampuni ijulikanayo kwa
jina la “Karanga leather Industries Co Ltd”
iliyoanzishwa mwaka 2017 kwa lengo
la kutekeleza mradi wa viwanda vya bidhaa za ngozi katika eneo la gereza la
Karanga , kampuni hiyo iliingia ubia kati
ya uliokuwa mfuko wa Pensheni PPF ambapo kwa sasa majukumu yake
yamechukuliwa na PSSSF pamoja na Jeshi la Magereza kupitia Shirika la
Uzalishaji. Malengo ya ubia huo nikuongeza wigowa uzalishaji wa bidhaa za ngozi
na kuongeza thamani ya ngozi nchini.
No comments:
Post a Comment