Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe akizungumza na washiriki wa Jukwaa
la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye
vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29,
2019.
Mwakilishi wa UN Women Nchini, Bi.
Hodan Addou akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari
Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari,
lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwandishi wa Habari Mkongwe,
Pili Mtambalike akichangia mada katika Jukwaa la Waandishi wa Habari
Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari,
lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe, akikata utepe kuzindua kitabu cha
Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari katika
jukwaa la Waandishi wa habari wanawake, lilifanyika Jijini Dar es Salaam
leo Novemba 29, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe na Mwakilishi wa UN Women nchini,
Bi. Hodan Addou, wakionyesha nakala ya kitabu cha Masuala ya unyanyasaji
wa kijinsia kwenye vyombo vya habari, kilichozinduliwa na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Jukwa la Waandishi wa Habari
Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwakilishi wa UN Women nchini,
Bi. Hodan Addou, akiandika anayoyasikia wakati wa Jukwaa la Waandishi wa
Habari Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
……………………
Na Judith Mhina -Maelezo
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrisom Mwakyembe amezindua kitabu cha Gender and Media Handbook in Tanzania wakati wa maadhimisho ya miaka
miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano.
Akizindua kitabu hicho katika
ukumbi wa Kibo ndani ya hoteli i ya Kimataifa ya Hyatt Regence – The
Kilimanjaro leo Jijini Dar-es-salaam Waziri Dkt Mwakyembe amesema “Wana
habari mtakuwa vibarua mpaka lini”.
Hebu tujaribu kutekeleza sheria
mbili ya Habari na ile ya haki ya kupata taarifa, ambapo Tanzania ni
kati ya nchi chache ambazo zimeiga kiila kitu kilichoandikwa kwenye
sheria husika ya kimataifa, badala yake wanaleta mada yao pendwa ya
jinsia moja, hatuwezi kukubali. Amesema Waziri Mwakyembe.
Akijibu risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano- Tanzania Women Media and Public Relation Networ,.
Bevin Bhoke Chacha Mwita ambaye amesema kuwa waandishi wa habari
wanawalke wananyanyaswa kijinsia katika vyumba vya habari . Hii ikiwa
ni pamoja na kutolipwa mshahara stahiki kulingana na sifa walizonazo,
kutopandishwa madaraja, lugha chafu na kubaguliwa katika majukumu ya
kazi kama waandishi wa kiume na kujikuta wengi wao wakiwa waadhirika wa
kunyanyaswa kijinsia.
Waziri mwakyembe aliongeza kwa
kusema “Tunaomba wahisani watenge nusu ya fedha wanazotoa ili kuangalia
masilahi ya waandishi wa habari na kuboresha mazingira ya kazi kutokana
na kuwa na vitendea kazi duni katika vyombo vyao vya Habari.
Ninashangaa waandishi wa Habari
ambao wanashangilia kuwa na taaluma isiyo na mpangilio, sheria wala
kanuni, katika kuimarisha taaluma yao na ndio maana leo hii mnalalamika
masilahi madogo yasiyolingana na kazi mnayofanya au hatopata mishahara
kabisa .
Akisisitiza jambo hilo Waziri
amesema “Ni agfadhali kuwa na vyombo vya Habari vichache vinavyojali na
lulinda masilahi ya Waandishi wa Habari kuliko kuwa na vyombo vingi
ambavyo , haviangalii masilahi ya waandishi wa Habari, kuwalipa
mishahara stahiki kwa wakati .
Akitoa agizo kwa kukabiliana na
suala la kupiga vita unyanyasaji kijinsia Waziri Mwakyembe amesema kuwa
nimefurahi kwa kuwa mmeonyesha namba mbili maalum za simu ambazo
yeyote atakayenyanyaswa kijinsia azipige ili kupata msaada. Aidha,
Wizara yangu naiagiza kuwa na namba maalum ya simu ambayo mtanipigia
mimi moja kwa moja na kuwatangaza wale wote wanaomnyanyasa wanahabari
wanawake ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha
vitendo vya unyanyasaji kwenye vyumba vya habari.
Akisisitiza agizo hilo amesema
dirisha la Waziri lipo wazi kwa kila mtu bila mashariti yeyote na naomba
wanahabari walitumie kweli kweli, mimi nikiwa kama mzazi na kiongozi
ni lazima kuhakikisha suala hili linakuwa historia.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa wanahabari wanawake na maafisa uhusiano Bi Chacha ameongeza kwa kusema kuwa wanawake wana
Katika hizi siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia katika vyumba vya Habari Mshauri wa masuala ya
wanawake wanahabari Bi Pili Mtambalike amesema “Wanahabari wanawake
wananyanyaswa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa kupewa kazi
nyepesi ikilinganiswha na waandishi wa kiume katika vyombo vya habari
kutokana na kutokujiamini
Aidha , katika vyombo vingi vya
Habari utafiti unaonyesha kuwa wahariri wengi ni wa jinsia ya kiume
japo wapo wanawake ambao wanastahili kuwa wahariri na wanalingana hata
kwa taaluma walizonazo ila hawapewi madaraka na hata hawapandishwi
madaraja kama wenzao wa jinsia ya kiume.
Vilevile waandishi wanahabari
wachanga wakike wananyanyaswa kingono na waliowengi wanafanya kazi
kwenye vyombo hivyo kama correspondence na kulipwa kulingana na stori
ambayo haiwatoshelezi kimaisha. Pia, Lugha wanazotumia wahariri katika
vyumba vya habari ni lugha chafu za kudhalilisha na vitisho.
Akiongelea upande wa pili kama
ushauri kwa wanahabari wachanga wanawake amesema kuwa ipo tabia ya
wanahabari hawa wa kike wachanga kujiendekeza ili wapate wepesi wa
kufanya kazi bila kuwa wabunifu kujituma na kuhakikisha wanajifunza
kila mara ili kukomaa kitaaluma.
Pili Bi Mtambalike amesema kuwa
ipo haja ya kuwa na sera ya jinsia katika vyombo vya Habari na
kuhakikisha sera hizo zinatumika . Utafiti uliofanywa katika vyombo 23
vya Habari sita tu ndio vilikuwa na sera inayoeleweka ambayo haitumiki.
Hivyo tunaomba Jukwaa la Wahariri
Tanzania –TEF liangalie namna gani linaweza kuleta usawa wa kijinsia
katika kuwa na idadi sawa ya wahariri kwa kuwa wanawake walio wengi
wanaishia katika ngazi ya Wahariri wasaidizi . Akitoa Takwimu amesema
asilimia 26 ya wanawake ndio wahariri wasaidizi waliosalia wote ni
jinsia ya kiume wakiwemo wahariri wakuu wa jinsia ya kiume.
Pia, unyanyasaji huu wa wanawake
unafanyika hata kwenye upande wa vyanzo vya Habari ambavyo kwa wanawake
ni asilimia 36 ,a silimia 64 ya vyanzo vya Habari hutokana na wanaume.
Hivyo tunaomba hata wanawake wanahabari walione hili na kuhakikisha
wanawahoji wanawake wenzao kama chanzo cha Habari badala ya kujikita
zaidi kwa wanaume. Amesema Bi Mtambalike.
Naye Mhariri Mtendaji Bakatri
Machumu ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo na kuwasilisha
taarifa yake kupitia video iliyorekodiwa amesema kuwa kutokana na uzoefu
wangu katika tasnia ya Habari waandishi wanawake ni wabunifu na
wananafasi kubwa ya kuangalia wanawake ambao wako katika jamii na
kusaidiana.
Naye Muwakilishi wa Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania Bibi Hodan Addou amesema “ Vyombo vya Habari ni
kati ya vyombo vyenye nguvu kubwa hivyo vitumike katika kuhakikisha
vinaondoa kabisa suala zima la unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia
katika vyomvo vya Habari”.
Pia, ameongeza kwa kusema kuwa ni
lazima kuhakikisha wanahabari wanawake wanashiriki kikamilifu katika
kuhakikisha wanatumia taaluma yao bila vikwazo ili kuwaletea maendeleo
mtu momoj ammoja na Taifa kwa ujumla.
Akiongelea kauli mbiu ya mwaka
katika maadhimisho ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake
Tanzania na Maafisa Uhusiano. Unaosema “Changamkia Fursa sasa” Grabbing Opportunity now
Katibu wa Kamati Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa
Uhusiano, Bi Leah Mushi amesema nafasi za mafunzo ambazo hutolewa na
wadau mbalimbali wa sekta wa Habari wakiwemo Wanawake wa Umoja wa
Mataifa, pamoja na Shirika la Mitandao ya Habari- Internews.
Aidha, kuna fursa nyingi za
mafunzo ya Mitandao ya kijamii na pia wanatoa vitendea kazi kwa
waandishi wachanga wake kwa waume ili waweze kujitegemea katika kufanya
kazi zao na kujiendeleza kitaaluma.
Naye Afisa Uhusiano wa Kituo cha
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bi Stela Vuzo, amesema kuwa huu ni
wakati muafaka kwa wanahabari wachanga wanawake Tanzania kuchangamkia
fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili ya kusimamia taaluma ya Habari na
kujiendeleza, ikiwa ni pamoja na kupata kazi sehemu mbalimbali duniani
na kuacha kulalamika kuhusu masilahi na mishahara midogo.
Haya tunayoyaona sasa
inatokana na mfumo dume ambao tumeuishi kwa miongo kadhaa ambayo adhari
zake zinajitokeza , hivyo sio kitu cha ajabu katika jamii zetu, na
hayatokei kwenye tasnia ya Habari peke yake bali ni mfumo wa malezi
kwenye jamii zetu ambao unatakiwa ukemewa, upigwe vita na uache kubagua
mtoto wa kike na yule wa kiume. Amesema Mhariri Jesse Kwayu.
Iko haja ya Wadau wa Tasnia ya
Habari kuongeza kwa pamoja na kuona umuhimu wa sheria , kanuni na
taratibu tulizojiwekea ili kuifanya sekta ya Habari iwe na mfumo
madhubuti unaowafaidisha wana taaluma ya Habari kwa jumla.
No comments:
Post a Comment