
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti Anitha Msangi (wa tatu kulia) akiongea na waandishi wa habari
wakati wa kutangaza maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya
kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial
Guinea. Wa kwanza kulia ni Haji Manara, mwenyekiti wa kamati ya
uhamasishaji akifuatiwa na Katibu Mkuu wa TFF Kidau Wilfred na wa kwanza
kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa Stars supports, Godson Karigo.

Katibu Mkuu wa TFF Kidau Wilfred
(kulia), akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza maandalizi
ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya
Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea. Kulia kwake ni Meneja
Masoko wa kampuni ya Bia ya Serengeti Anitha Msangi akifuatiwa na Haji
Manara, mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji na Cliford Ndimbo, Afisa
habari wa TFF.

Waandishi wa habari kutoka vyombo
mbali mbali vya habari, wakifuatilia mkutano wa kutangaza maandalizi ya
Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika
(AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea utakachezwa jijini Dar es Salaam
November 2019.

Mwenyekiti wa kamati ya
uhamasishaji ya Taifa Stars Haji Manara (wa pili kulia) akiongea na
waandishi wa habari wakati wa kutangaza maandalizi ya Taifa Stars
kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021)
dhidi ya Equatorial Guinea. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF
Kidau Wilfred akifuatiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti
Anitha Msangi Na kushoto ni Afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo.
………………………..
Na Mwandisdi Wetu
Mdhamini mkuu wa Timu ya Taifa
(Taifa Stars) Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kupitia bia
yake ya Serengeti Premium Lager, imeahidi kuendelea kuwapa raha wapenzi
wa
soka hapa nchini kupitia udamini wake kwa Timu ya Taifa.
Taifa Stars, inatarajia
kucheza mechi yake ya kufuzu tiketi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea Novemba 15 katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa
kutangaza maandalizi kuelekea mechi hiyo, Meneja Masoko wa SBL Anitha
Msangi alisema SBL kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager ipo bega
kwa bega na Timu ya Taifa pamoja na mashabiki wa soka.
“SBL kupitia bia yetu ya
Serengeti Premium Lager tutataendelrea kuwapa burudani mashabiki wa soka
kwa kuhakikisha tunaiwezesha timu yetu ya taifa kufanya vizuri lakini
pia kupitia bia ya Serengeti kuwafanya mashabiki wafurahie mechi pamoja
na bia yao pendwa,” alisema
Anitha alisema, ili
kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanafurahia mechi hiyo, kampuni ya
SBL itaweka skirini kubwa sehemu mbali mbali ambazo zitaonyesha mechi
bure huku nafasi ya kufurahia bia ya Serengeti ikitolewa.
“Tujitokeze kwa wingi kuishangia timu yetu huku tukifurahia bia yetu ya Srengeti Premium Lager ambayo ni fahari yetu,” alisema
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kidau Wilfred alisema timu itaingia
kambini hivi karibuni kujiandaa na mchezo huo wa nyumbani..
Kidau alifafanua kuwa, mchezo
wa pili wa kufuzu AFCON utachezwa ugenini ambapo Stars wataenya na Libya
Novemba 19,2019, siku 4 tu baada ya kucheza mchezo wa kwanza.
“Tunawaomba Watanzania kwa
pamoja tuungane kwa ajili ya timu yetu ya Taifa. Tujitokeze kwa wingi
siku ya mechi na kuishangilia kwa nguvu zetu zote ili kuwapa hamasa
wachezaji wetu waweze kufanya vizuri,” alisema Ndimbo.
No comments:
Post a Comment