
Cornel Magembe akipokea vitanda na
mashuka kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Abraham Augustino
(aliyevaa suti), wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika juzi
wilayani Ukerewe. Benki hiyo imekabidhi msaada wa vitanda na mashuka
kwa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe, viti na meza za shule na chuo cha
Murutunguru,vifaa vya ujenzi kwa Zahanati ya Bwasa na shule za msingi na
Sekondari za wilaya ya Ukerewe vyote vikiwa na thamani ya shilingi
milioni 75.

Sospeter Magese, Akikabidhi msaada
wa Bati za Shule za Sekondari na Msingi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora
Erick Komanya. Benki ya NMB ilikabidhi viti na meza kwa shule za
sekondari, vifaa vya unjenzi – bati 216, mbao na misumari kwaajili ya
shule za msingi Kanyenye, Kalunde na Ikomwa vyote vikiwa na thamani ya
shilingi milioni 30.

Siriel Mchemba (Mwenye miwani)
akipokea moja ya vifaa tiba kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki
– Baraka Ladislaus kwa ajili ya kituo cha afya Gairo mkoani Morogoro.
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Gairo, Agnes Mkandya na Mganga M.fawidhi wa kituo cha afya Gairo, Dk.
Dastan Mshana.

Janeth Shango akikabidhi msaada
wa bati 175 kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea- Pololet Mgema kwa niaba ya
shule ya Msingi Ndelenyuma katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.
………………
NA MWANDISHI WETU
KATIKA kuunga juhudi za utatuzi wa
changamoto zinazoikabili Sekta ya Afya na Elimu nchini, Benki ya NMB
wiki iliyopita ilikabidhi misaada mbalimbali yenye thamani ya
Shilingi
Milioni 110 katika wilaya za Songea, Tabora na Ukerewe.
Thamani ya misaada hiyo ya vifaa
vya ujenzi na vifaa tiba, vinaifanya Benki ya NMB kutumia zaidi ya Sh.
Mil. 900 kununulia na kukabidhi vifaa hivyo kwa Shule za Msingi,
Sekondari, Zahanati na Vituo vya Afya nchini kwa mwaka huu. – 2019
Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza,
NMB imekabidhi misaada ya vifaa vya ujenzi, elimu na afya yenye thamani
ya Sh. Mil. 75 kwa shule 14 za msingi na sekondari, Chuo cha Ualimu
Marutunguru na Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.
Msaada huo, ulitolewa na Meneja wa
NMB Kanda ya Ziwa, Augustino Abraham na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya
hiyo (DC), Corneli Magembe, ambaye aliishukuru benki hiyo kwa uwezeshaji
huo, alioutaja kama unaoenda kumaliza tatizo la uhaba wa vifaa kwa
taasisi husika.
Mkoani Tabora, NMB imekabidhi viti
na meza wenye thamani ya Sh. Mil. 30 kwa shule sita za Manispaa ya
Tabora, tatu zikiwa ni za sekondari na nyingine tatu za msingi, msaada
ambao ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Erick Komanya.
Hafla hiyo ilifanyika Sekondari ya
Wavulana Tabora, ambako Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter
Magese, alikabidhi mabati 216, mbao na misumari vyote vikiwa na thamani
ya Sh. Mil. 15, kwa ajili ya Shule za Msingi Kanyenye, Kalunde na
Ikomwa.
Aidha, NMB ikatoa msaada wa mabati
175 ya geji 28, yenye thamani ya Sh. Mil. 5, kwa ajili ya Shule ya
Msingi Ndelenyuma, iliyopo katika Halmashauri ya Madaba, wilayani Songea
mkoani Ruvuma.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
bati hizo katika hafla ambayo ilifanyika katika Shule ya Msingi
Ndelenyuma, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Janeth Shango, alisema kwa
miaka kadhaa sasa NMB imekuwa mstari wa mbele kuchangia miradi ya
mbalimbali ya maendeleo.
“Mpaka ninavyoongea leo, kwa mwaka
huu 2019 pekee, tayari NMB tumetoa misaada yenye thamani ya Shilingi
Milioni 900, tumejikita zaidi kwenye miradi ya elimu, afya na majanga,”
alisema Shango wakati wa hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika
wilayani Songea.
No comments:
Post a Comment