Mkurugenzi
wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),
Dkt. Abdulsalaam Omary, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo ya siku moja
kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa wanachama wa Chama Cha
Waajiri Tanzania (ATE) jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka |
Mtaalamu wa TEHAMA, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Mihayo Mathayo, ya huduma zitolewazo na Mfuko kupitia Mtandao (Self Service Portal)
Meneja Madai Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao yatolewayo na WCF.
Kutoka
kushoto, Meneja Madai WCF, Bi. Rehema Kabongo, Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano ya Umma na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, Mwanasheria wa
Mfuko, Bw. Deo Ngowi na Bw. Pascal Richard kutoka kitengo cha Usajili
na Uwasilishaji Michango WCF, wakinakili hoja na maswali yaliyoelekezwa
kwenye Mfujo na washiriki, wakati wa majadiliano.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MABORESHO makubwa ya utoaji taarifa
za ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi kwa kutumia mtandao “e-notification” yamelenga kusogeza
karibu kabisa huduma za Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) kwa wadau wake na
hivyo kuongeza tija, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam
Omary amewaambia wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) wakati wa semina
ya mafunzo ya siku moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Kwa sasa wadau wa
Mfuko ambao wanatumia huduma za mtandao hawalazimiki kufika kwenye ofisi zetu
ili kuhudumiwa, bali wanaweza kupata huduma hizo kutoka mahala popote na wakati
wowote na tunaamini hatua hii imepunguza gharama na kuokoa muda ambao
utaongeza uzalishaji na hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa
ujumla.” Alisema Dkt. Omary ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw.
Masha Mshomba, katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama Cha
Waajiri Nchini (ATE).
Dkt. Omary alisema Mfumo huu
unamwezesha Mwajiri kutoa taarifa ya tukio kwa wakati kuwasilisha nyaraka na
kujua hatua iliyofikiwa katika uchakataji wa madai ya fidia kwa njia ya
mtandao.
Mfuko umetoa fursa kwa wateja wake
kupata huduma mbalimbali kupitia mifumo ya kielektroniki (TEHAMA), alisema.
Akiwasiklisha mada ya jihudumie
kupitia mtandao (Self Service Portal) Mtaalamu wa TEHAMA, wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF), Bw. Mihayo Mathayo alisema Mifumo hiyo iliyosimikwa ni
pamoja na Mfumo wa Usajili ambao unamuwezesha mwajiri kujisajili
(e-registration) na kupata hati ya usajili papo hapo, anafafanua mtaalamu wa IT
kutoka WCF, Bw. Mihayo Mathayo.
Bw. Mihayo alitaja Mifumo mingine
kuwa ni pamoja na Uwasilishaji michango ambao unamwezesha Mwajiri kutnza
taarifa za wafanyaakazi na kuwasilisha michango kupitia nambari ya udhibiti
yaani Control Number na kupata
stakabadhi ya kielektroniki.
“Jambo la kufurahisha, mteja utatumia
si zaidi ya dakika tano kupata huduma ukitumia mfumo huu wa TEHAMA, na hivyo
kuleta tofauti kubwa sana na hapo awali ambapo kwanza mteja analazimika kufunga
safari na kuzifata ofisi za Mfuko ili kuhudumiwa na hivyo kusababisha upotevu
wa muda.” Alifafanua Bw. Mihayo.
Kwa upandew
wake, MKURUGENZI Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt. Aggrey
Mlimuka, aliushukuru uongozi wa WCF kwa kutenga muda wao kutoa elimu hiyo
muhimu kwa wanachama wake, kwani itasaidia sana katika utekelezaji wa majukumu
yao.
Mbali na kujifunza masuala hayo ya
huduma zitolewazo na WCF kupitia Mtandao, washiriki hao pia walipatiwa mafunzo
mbalimbali yakiwemo Sheria iliyoanzisha Mfuko, Kujisajili na jinsi ya
kuwasilisha michango WCF na namna ya kuwasilisha madai ya Fidia na Mafao
yanayotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment