Pages

Monday, November 4, 2019

LITAKUWA JAMBO JEMA KAMA MABARAZA YA FAMASIA KATIKA NCHI ZA SADC YATAANZISHA USHIRIKIANO WA KITAALUMA HAPO BAADAE KAMA ILIVYO KWA EAC


Msajili wa Baraza la Famansia nchini, Elizabeth Shekalaghe akizungumza na waandishi wa habari katika banda la baraza hilo kando ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za SADC unaofanyika kwenye ukimbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Msajili wa Baraza la Famansia nchini, Elizabeth Shekalaghe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa baraza hilo  katika banda la baraza hilo kando ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za SADC unaofanyika kwenye ukimbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
……………………………………………
Msajili wa Baraza la Famansia nchini, Elizabeth Shekalaghe amesema baraza hilo linashiriki katika ...mkutano wa mawaziri wa afya na UKIMWI wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya SADC kuona ni mambo gani yatakayojadiliwa katika mkutano huo ili na wao waone namna nzuri ya kuibua hoja ya wataalamu wa mabaraza ya famasia katika nchi hizo watakavyoanzisha ushirikiano na kubadilishana utaalamu hapo baadaye.
Bi. Elizabeth Shekalaghe ameyasema hayo katika banda la baraza hilo kwenye maonesho yanayoendelea kando ya mkutano wa mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za SADC unaofanyika kwenye ukumbi wa  Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Amesema kwa upande wa Mabaraza ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kumekuwa na ushirikiano mkubwa kwa wataalam wa Famasia wa nchi hizi ili kuhakikisha dawa haziuzwi wala kutolewa kiholela kwa watumiaji.
“Kama wataalamu wa Famasia katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)mabaraza yetu yamekuwa yakikutana na kufanya vikao mbalimbali ili kujadili changamoto zinazowakabili wataalamu wa Famasia na kuona ni namna gani tunaweza kupiga hatua katika utaalamu wa huduma hiii muhimu katika afya”. Amesema Bi. Elizabeth Shekalaghe
Ameongeza kuwa kama wataweza kuanzisha ushirikiano huo kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za SADC pia  hapo baadae itakuwa ni hatua muhimu sana kufikiwa kwani itaweza kuongeza wigo wa kubadilishana uzoefu na utaalam wa shughuli za wafamasia katika mabaraza ya nchi za ukanda huo.
Hapa nchini sheria inataka kila duka la famasi kuwa na mtaalamu wa  famasia mmoja. hivyo wafamasia ni humuimu sana serikalini pamoja sekta binafsi katika huduma ya afya ,  takwimu zinaonesha  mwaka 2013 kulikuwa na wafamasia 350 na kufikia mwaka jana wamefikia wafamasia 1400 jambo ambalo linaonesha umuhimu wa kuwepo kwa wataalamu wa famasia na wanatakiwa kuongezeka zaidi ili kuboresha mazingira ya huduma hii.
 

No comments:

Post a Comment