Mkurugezi wa Kurugenzi ya Huduma
kwa Umma Dkt. Mona Mwakalinga, pamoja na Dr. Fikira Kimbokota wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa wakifuatilia jambo wakati wa mafunzo
hayo chuoni hapo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
(Taaluma, Tafiti na Ushauri) Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. A Makuliko na
Prof. A Mtembei wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakiteta jambo wakati wa
Mafunzo yanayoendelea katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa.(
MUCE)
Baadhi ya
wanataaluma wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Kupata Makala kutoka
katika Tasnifu zao yaani (How to turn a Thesis / Dissertation into a
Journal Article). Yaliyoandaliwa na Kurugenzi ya Huduma kwa Umma kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mmoja wa
wanataaluma wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, akiuliza jambo
wakati wa mafunzo Kupata Makala kutoka katika Tasnifu zao. (How to turn
a Thesis / Dissertation into a Journal Article).
*******************************
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
kimetoa mafunzo ya Siku tano kwa wafanyakazi wanataaluma wa Chuo Kikuu
Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) Mkoani Iringa, jinsi ya Kupata Makala
kutoka katika Tasnifu zao. (On How to turn a Thesis/Dissertation into a
Journal Article). Mafunzo hayo yalianza rasmi tarehe 2 Novemba 2019 na
yanatarajiwa kumalizika tarehe 5 Novemba, 2019.
No comments:
Post a Comment