
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumza na Washiriki kutoka Taasisi
mbalimbali nchin wakati wa mkutano wa majadiliano ya wiki ya Azaki
yanayoendelea jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini waliojitokeza katika mkutano wa wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma.

Mratibu wa Asasi zisizo za
kiserikali kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw.akichangia mada wa mkutano
wa majadiliano ya wiki ya AZAKI inayoendelea jijini Dodoma
………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKURUGENZI mtendaji wa taasisi ya
Twaweza Aidan Eyakuze,amesema kuwa Asasi 16 za
Kiraia (AZAKI) nchini kwa
utafiti uliofanywa umesaidia kutoa mchango wa sh.Bilioni 236 kwenye
uchumi wa nchi ndani ya miaka mitatu 2016 hadi 2018.
Hayo ameyasema wakati alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha mada ya
mchango wa Asasi za kiraia kwenye uchumi wa nchi, ikiwa ni sehemu ya
maazimisho ya wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma
Amesema kuwa kiasi hicho cha
fedha kilichopatikana kutokana na Asasi za kiraia kwa kipindi cha miaka
mitatu ni sawa na kilo 2,181 za dhahabu zinazosafirishwa na kuuzwa nje
ya Nchi.
“Lakini pia kiasi hicho cha
fedha ambacho kimechangiwa na Asasi hizi 16, kwa kipindi hicho cha miaka
mitatu ni sawa na serikali kuingiza watalii 42,316 na kukaa nchini kwa
muda wa wiki moja au ni sawa lita 247 milioni za petrol,dezeli na mafuta
ya taa” Amesema Eyakuze.
Pia Eyakuze amesema kuwa katika
kipindi cha miaka mitatu 2016/18 kiasi cha kodi ambazo zimelipwa na
Azaki hizo 16 kwa serikali ni kiasi cha Sh. Bilioni 19.
Amefafanua kuwa kiasi hicho cha
kodi kilichokusanywa kwa kipindi hicho ni sawa na mapato yatokanayo na
maji ya kunywa, vinywaji laini na sigara ya mwaka 2018/19 ambayo
yalikuwa ni bilioni 18.8.
“Au kiasi hicho cha kodi
kilichokusanywa unaweza kulinganisha kabisa na kodi iliyokusanywa na
Mamalaka ya maopato nchini TRA 2018/19 katika mikoa ya Rukwa, Lindi,
Simiyu, Songwe na Katavi kwa pamoja ambayo makusayo yao ni Sh. Bilioni
21,” Amesema Eyakuze.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Foundation For Civil Society Francis Kiwanga, amesema katika wiki hiyo
ya Azaki moja kati ya shuguli zitakazofanyika ni pamoja na kuwa na
kongamano linalojumuisha wadau wengine ikiwemo serikali.
Amesema katika kongamano hilo
wanajadiliana namna ya kushirikiana na kuweka mikakati ili mchango wa
Asasi za kiraia uweze kutambulika na serikali.
Awali Mratibu wa Asasi za kiraia
nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali a mitaa
(Tamisemi) Denis Londo amesema Asasi la Kirai zinamchango mkubwa kwa
Taifa.
No comments:
Post a Comment