Pages

Tuesday, October 29, 2019

Waziri wa Nishati akagua mradi wa umeme wa Julius Nyerere



**********************************
Na Hafsa Omar – Rufiji
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amekagua mradi umeme wa Rufiji (MW 2115) akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nyumba wa Misri, Mahmoud Nassor ambapo pia
walifanya Mazungumzo kuhusu mradi huo unaofanyika wilayani Rufiji.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Oktoba 27, 2019, Dkt Kalemani amlihakikishia Waziri huyo wa Misri kuwa, Serikali ya Tanzania itahakikisha mradi huo unamalizika kwa muda uliopangwa kwa kumsimamia vizuri mkandarasi na kuhakikisha kila kinachohitajika katika mradi huo kinapatikana kwa muda muafaka.
Aidha, Dkt Kalemani alieleza kuwa, Serikali ya Tanzania haitarajii kutokea kwa sababu yoyote itakayochelewesha mradi huo na kumhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa, wakandarasi watalipwa kwa wakati.
Alifanunua kuwa, mradi huo hadi sasa utekelezaji wake umefanyika kwa miezi 10 kati ya miezi 42 aliyopewa mkandarasi ili kukamilisha kazi husika, “ni matumaini yetu kazi zote zitakamilika kwa wakati na nimetembelea mradi nimeona utekelezaji unaendelea vizuri, upo ndani ya muda kama mkataba unavyoelekeza.”
“ Nataka nitoe rai kwa mkandarasi kuwa tarehe 14 Juni 2022 awe tayari amemaliza shughuli zake zote na mradi ukamilike kwa mujibu wa mkataba.”Aliongeza Dkt. Kalemani
Katika kuhakikisha kuwa, maji yanapatikana muda wote katika mradi huo, Waziri Kalemani alisema kuwa mwezi Mei mwaka huu aliunda timu ya uratibu wa shughuli ya utekelezaji wa mradi ambapo ameiagiza timu hiyo na Taasisi zinazohusika zianze kupita Mkoa kwa Mkoa, ili kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nyumba nchini Misri ambaye pia ndio msimamizi wa masuala ya mradi huo, Mahmoud Nassor, alisema mradi huo umefanikiwa kwa sababu wanapata ushirikiano wa Waziri na Nishati pamoja na wasimamizi wa mradi huo.
Aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa ushirikiano huo na kueleza kuwa mradi huo ni rafiki wa mazingira kwani hautayaharibu

No comments:

Post a Comment