TGNP
Mtandao imepanga kufanya mapitio ya sera na ilani za vyama vya siasa
kwa mrengo wa kijinsia na kushauri kufanya marekebisho mapema kabla ya
uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Viongozi
mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo wakiwa katika picha ya pamoja na
wageni wao kutoka TGNP Mtandao, wakionesha Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2019 iliyotengenezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau wengine
wa haki za wanawake.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukabidhi ilani ya madai ya wanawake katika uchaguzi
wa serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa
chama cha ACT wazalendo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian
Liundi, alisema kwamba baada ya kutembelea vyama kadhaa vya siasa nchini
na kusikiliza jinsi wanavyotekeleza masuala ya kijinsia, ameona kuwa
kuna haja ya TGNP na Mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na
Usawa wa Jinsia, kufanya uchambuzi au mapitio ya sera na ilani za vyama
kwa mrengo wa kijinsia na kuangalia mapengo ili kushauri marekebisho.
“Tunapoelekea
uchaguzi wa seriali za Mitaa, na uchaguzi mkuu mwaka ujao 2020,
tunahitaji vyama hivi kuzingatia kwa kiasi kikbwa usawa wa kijinsia
kwenye uteuzi wa wagombea. Kama chama hakina sera za ndani ambazo zina
mrengo wa kijinsia, ni lazima mapendo yataendelea kuwepo. Tunashukuru
kwamba vyama vya siasa vimejitahidi, lakini bado hatujafikia malengo”
Alisema.
Kwaupande
wake Kaimu Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Doroth Sembu alisema
kwamba, pamoja na kwamba chama kinajitahidi kutoa fursa sawa kwa
wanawake bado watajitahidi kuendelea kuteua wanawake kushiriki kwenye
chaguzi.
“mwaka
huu tumejipanga kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, tutahakikisha
kila mahali ambapo wanawake wamejitokeza wanapata nasi, lakini kwa
sababu mmetuletea hii Ilani yenu, tutahakikisha tunaitumia ili wagombea
watakao shinda wakatekeleze ilani husika” alisema Semu
Ilani
ya Madai ya wanawake kwa uchaguzi wa serikali za Mitaa 2019 na
Uchaguzi Mkuu 2020 iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na
Mtandao wa wanawake na Katiba, imewashirikia na kukusanya maoni ya
wanawake kutoka katika makundi yote nchini hasa vijijini. Asasi za
kiraia zinazotetea haki na usawa wa Kijinsia zaidi ya 60 zimeshiriki.
No comments:
Post a Comment