Pages

Tuesday, October 29, 2019

MZEE ANAEKADILIWA KUWA NA MIAKA ZAIDI YA 80 AUWAWA NA WANAFUNZI KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA



Mzee Issa Pela Mkazi wa Kijiji cha uganga wilayani makete mwenye umri wa miaka 80 amefariki dunia baada ya shambulio la fimbo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi kwa
tuhuma za uchawi ambao unaaminiwa kusababisha walimu na wanafunzi kudondoka na kuzimia.
Kwa mijibu wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi luganga Eliuda Msigwa mapema  asubuhi majira ya saa nne octoba 28 mzee issa alifika shuleni hapo na kuanza kufanya matukio yanayoashiria vitendo ya ushirikiana ikiwemo kuchora misalaba chini ya ardhi na kuchuma majani na ndipo wanafunzi wachache wanaofikia 15 kwa idadi wakaanza kumshambulia kwa kutumia fimbo mpaka mauati yakamkuta.
Mtendaji wa Kijiji cha uganga ameeleza kuwa Kijiji hicho kinazungukwa na idadi kubwa ya watu wanaotuhumiwa na ushirikina hali mabayo inawakwamisha shughuli za maendeleo ikiwemo ustawi wa elimu ambapo mpaka kufikia tukio la ushambuliwa mzee huyo shughuli za masomo zilikuwa zimesimama kutokn na walimu na wanafunzi kukumbwa na vitisho mbalimbali ikiwemo kudondoka na kuzimia ovyo kwa wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo wakiwemo waliohusika na tukio hilo wamesema kuwa baada ya kumcharaza kwa fimbo mzee huyo alikiri kuhusika na vifo vya watu watatu kijijini ambao aliwaloga na baadae mauti yakamkuta kutokana na kichapo.
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Uganga Frank Gavana amethibitisha kutokea kifo hicho baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu ambapo amesema majeraha ya sehemu za kichwa cha marehemu ni sababu kubwa iliyopelekea kifo chake.
Jeshi la polisi wilaya ya Makete limefika eneo la tukio na kutoa elimu kwa jamii na kuonya tabia za kuchukua sharia mkononi ambapo hata hivyo halijamkamata mtu yeyote kuhusika na mauaji hayo
Juhudi za kumpata kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Hamisi Issa kuzungumzia tukio hilo zinaendelea ambapo awali kwa njia ya simu alisema taarifa hizo hazija mfikia

No comments:

Post a Comment