Pages

Wednesday, October 2, 2019

MARUFUKU KUFANYA KAZI YA KUCHUNA NA KUHIFADHI NGOZI BILA KUWA NA LESENI



Marufuku Kufanya kazi ya kuchuna,kuwamba na kuhifadhi ngozi,bila kuwa na leseni au
kusajili eneo la biashara ya ngozi.
Haya yamebainishwa leo jijini Arusha na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo na Usalama wa chakula Bw.Gabriel Bura wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa wachunaji.

”Hivyo ni marufuku kuchuna,kuwamba au kuendesha biashara ya ngozi katika eneo husika bila kuwa na leseni au kusajiliwa vinginevyo hatua kali zitachukuliwa kwa yule atakayefanya kazi ya ngozi bila kuwa na leseni au kusajiliwa kisheria”amesema Bw.Bura
Kaimu Mkurugenzi huyo ameitaja sheria inayomtia matatani atakaye fanya kazi ya ngozi bila kuwa na leseni au kusajiliwa eneo lake la kazi atashitakiwa chini ya Sheria ya ngozi namba 18 ya mwaka 2008.
Aidha kaimu mkurugenzi huyo,amesema wanaopata leseni na kusajiliwa ni lazima wapatiwe mafunzo kwanza kabla ya kuomba leseni na usajili wa taaluma ya teknolejia ya utayarishaji bora wa zao la ngozi.
Mkurugenzi huyo,ameendelea kuleza kuwa ni matarajio yake kuwa baada ya mafunzo haya anategemea makubwa kuhusu mabadiliko ya ubora wa zao la ngozi utakuwa na tija kulingana na ulewa wa wadau katika mafunzo waliyoyapata na hatimaye kuchangia kikamilifu katika pato la Taifa.

No comments:

Post a Comment