********************************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba,
Bukoba,
TAASISI ya kuzuia na
kupambana na rushwa Mkoa wa Kagera Jana ( Leo ) imemfikisha mahakamani
kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya Ranchi za Taifa ( NARCO ) kwa
kuomba
rushwa ya shilingi milioni 12.
Akiongea na waandishi wa
habari ofisini kwake Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera,Bw.John Joseph,
alisema kaimu meneja Mkuu wa kampuni ya Ranchi za Taifa ( NARCO
)Prof.Philemon Wambura amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Bukoba kwa
tuhuma za rushwa.
Bw.Joseph,alisema
Prof.Wambura anakabiliwa na tuhuma za rushwa ikiwa ni pamoja na kuomba
na kupokea rushwa ,matumizi mabaya ya ofisi,ubadhilifu na uhujumu
uchumi kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sheria namba
11 ya mwaka 2007.
Alisema taasisi hiyo
ikiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuzuia na kupambana na
rushwa Septemba 23 mwaka huu ilipata taarifa kutoka vyanzo vyake ambavyo
vilionyesha kuwa Prof.Wambura kaimu meneja Mkuu NARCO,amekuwa
akijihusisha na vitendo dhidi ya rushwa ikiwemo kuomba na kupokea rushwa
kutoka kwa baadhi ya wafugaji wenye uhitaji wa Vitalu vya kufugia
Ng’ombe wenye vitalu ambao wanahitaji kuhuisha mikataba yao ya awali.
Alisema taarifa ya
uchunguzi imeonyesha kuwa January 3, 2018 Prof.Wambura Prof.Wambura
akiwa kaimu meneja Mkuu wa NARCO alipokea kiasi cha shilingi milioni 12
kutoka kwa mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa ili aweze kumpatia
kitalu kwaajili ya kufanyia shughuli za ufugaji huku akifahamu kuwa
jambo hilo ni kosa na kinyume cha sheria.
Wakati huohuo alisema kuwa taasisi hiyo imewafikisha watu wengine wanne kwa makosa mbalimbali Octoba 25 mwaka huu.
Amewataka watu hao kuwa
ni Stanslous Katto mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari
Kashenye kwa makosa ya kugushi ,kujipatia mamlaka asiyokuwanayo na
kuwasilisha nyaraka zenye maelezo ya uongo kwa mkurugenzi wa halmashauri
ya Wilaya ya Missenyi kwa lengo la kujipatia kiasi cha shilingi milioni
5.7.
Alisema uchungunzi
ulibaini kuwa Juni 09,2015 Katto,alighushi alighushi sahihi ya
mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Bukwali jina linahifadhiwa na
kughushi sahihi ya mkandarasi pia jina linahifadhiwa na jina la kampuni.
Aliwataja wengine kuwa
ni Richard Kavogoro mwenyekiti wa Kijiji cha Mkalinzi ,Josephat Nzeye
mtendaji wa Kijiji cha Mkalinzi na Onesmo Tiara ambaye alikuwa
mwenyekiti wa Vocha za pembejeo wa Kata Muganza halmashauri ya Ngara.
Alisema wote
wamefikishwa katika mahakama ya wilaya Ngara kujibu tuhuma
zinazowakabili za kutumia nyaraka kwa lengo la kumdangaya mwajiri.
Alisema taarifa ya
uchunguzi imeonyesha kuwa zoezi la ugawaji wa Vocha za pembejeo kwa
wakulima msimu wa wa 2016/2017 kwa nyakati tofauti katika Kijiji cha
Mkalinzi Kata ya Muganza kulifanyika udanganyifu.
Alisema baadhi ya majina ya wanufaika sahihi zao zilighushwa ili kuonyesha kuwa wamepokea mbolea ya ruzuku wakati si kweli.
No comments:
Post a Comment