WAZIRI wa Madini Doto Biteko akizungumza na wananchi wa wilaya ya Tunduuru wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma |
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Waziri wa Madini Doto Biteko
MKUU
wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Julius Mtatiro akizungumza katikati
ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kulia ni Waziri wa Madini
Doto Biteko
WAZIRI
wa Madini Doto Biteko amewataka watu wanaotorosha madini hapa nchini
kwenda nchi za nje waache mara moja biashara hiyo kwani ni zilipendwa
badala yake wayapeleke kwenye masoko mbalimbali ili kuweza kuyauza.
Biteko
aliyasema hayo akiwa kwenye ziara yake mkoani Ruvuma ambapo alisema
kwamba badala yake wafanyabiashara hao kupeleka madini yao na wayauze
huku akieleza iwapo wanataka kibali cha kusafirisha madini watapata
ndani ya masoko hayo.
Alisema
kwamba unaweza kununua madini ukafungiwa na unaweza kusafirisha huku
akiwaomba viongozi wa serikali watu wa wizara ya madini, mamlaka
nyengine wawasaidie watanzania kunufaika na madini yao.
“Ndugu
zangu tusiwafanye watanzania wawe watoshaji wa madini tukiwa
tunawafuata kila wakati utawafanya watu wasifike kwenye soko na
wafurahie kufanya vitendo ambavyo sio vizuri “Alisema.
Waziri
Biteko pia aliwataka watanzania wajanja wajanja wanaotaka kuuza madini
feki teknolojia imekuwa hivi sasa hivyo wasijiingize kwenye matatizo kwa
maana hawatasalimika.
“Katika
mkoa wa Ruvuma na nchi ya Tanzania kuna maeneo yanayozalisha madini ya
vito kwa wingi ni Tunduru ipo na ni wilaya zinazozalisha vito kwa
wingi.. Tulikuwa tunafanya baishara kubwa lakini maisha ya watu wa
tunduru yalikuwa hayaonyeshi kama kulikuwa na maisha ya namna
hiyo”Alisema
“Madini
yalikuwa yanatoroshwa kupelekwa nje ya nchi lakini Rais wetu Dkt John
Magufuli akasema tufunge breki tuanzisha masoko ya madini hatua ambayo
imeweza kuwasaidia sana sekta ya madini hapa nchini “Alisema
Alisema
kwamba katika kumbukumbu zake mwezi February mwaka jana alikutana na
wageni wengi ambao wananunua madini kupitia leseni za wenyeji huku
wakiwapa kupewa fedha kiduchu jambo ambalo lilikuwa likiwaumiza
watanzania wengi.
Waziri
huyo alisema kwamba lakini Rais Dkt Magufuli akawataka watengeneze
utaratibu wa kusimamia madini hayo ili yaweze kuwa na manufaa kwa watu
wa tunduru na mkoa kwa ujumla.
“Watu
wa Tunduru wanahitaji fedha wajenge nyumba nzuri,fedha wasomeshe
watoto,wale vizuri wakae kwenye mazingra mazuri hata mtu akiihtaji kuoa
aweze kuona bila mkopo”Alisema
No comments:
Post a Comment