Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza jambo wakati wa
kikao cha majumuisho cha ziara ya kutembelea miradi ya uwekezaji katika
Wilaya ya Ruangwa mkoni Lindi pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (aliyekaa
kulia) kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji
madini ya Lindi Jumbo Paul Shauri akionesha michoro ya muonekano wa eneo
la mgodi wa madini aina ya uno (Graphite) wakati wa ziara ya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Bw.
Hashim Mgandilwa akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya
Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula katika ofisi zake Mkoani
Lindi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ruangwa Bw. Barnabans Essau akisalimia wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah
Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt.Angelline Mabula wakiwa katika ziara ya kukagua eneo lililotengwa
kwa ajili ya uchimbaji wa madini aina ya uno (Graphite) lililopo Wilayani Ruangwa Lindi Septemba 27, 2019.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment