Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
ametoa agizo kwa waajiri kote nchini kuendelea kuwapa likizo ya
kunyonyesha ndani ya siku 84 akina mama mara wanapojifungua kama
ilivyo kwa mujibu wa Sheria.
Waziri
Ummy ametoa maagizo hayo leo Agosti 1,2019 jijini Dodoma wakati wa
ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani ambayo
yameanza Agosti 1 hadi 7,2019.
Mhe.Ummy
amesema mama aliyejifungua ana haki ya kupewa likizo ya siku 84 hivyo
ni wajibu wa kila mwajiri kutoa likizo kwa waajiri na mwajiri anayekiuka
maagizo hayo ni mwajiri adui wa wanawake na watoto wa Tanzania na
serikali haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria.
Aidha,Waziri
Ummy amefafanua mchanganuo wa likizo ambapo amesema mama aliyejifungua
mtoto mmoja anapaswa kupewa likizo ya siku 84 na aliyejifungua mapacha
anastahili kupata likizo ya siku 100 ,baba mzazi ana haki ya likizo ya
siku tano huku pia akitoa tahadhari ya kuifuta sheria kwa akina baba
kwani baadhi yao wamekuwa wakitumia mwanya huo kushinda baa na vijiweni
badala ya kumsaidia mama.
Waziri Ummy ameongeza kuwa kanuni za utumiaji wa Maziwa ya watoto ya
kopo,maelekezo yanatakiwa kwa lugha zote mbili Kishwahili na kiingereza
ili mtu wa kijijini aelewe namna ya matumizi.
Pia
waziri Ummy amesema asilimia 31% ya watoto waliochini ya miaka 5
wamedumaa kutokana na kukosa maziwa ya mama huku akitaja baadhi ya
faida za unyonyeshaji kuwa ni pamoja na hali ya lishe kwa watoto kuwa
nzuri,kuondoa uwezekano wa saratani ya matiti na uzazi kwa akina
mama,kupungua udumavu na utapiamlo kwa watoto .
Kwa upange wake ,Mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto Duniani
[UNICEF]hapa nchini,James Gitau amesema asasi za kiraia zinapaswa
kuendelea kutengeneza mazingira ya Unyonyeshaji katika maeneo ya kazi
huku akiishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwawezesha wazazi
kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ya unyonyeshaji .
Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani hufanyika kila ifikapo
tarehe 1 hadi 7 ya kila mwaka na kaulimbiu mwaka huu ni “Wawezeshe
wazazi kufanikisha unyonyeshaji”huku takwimu zikionesha kuwa asilimia
97% ya watoto walio chini ya umri wa miaka 2 wananyonyeshwa maziwa ya
Mama na hali ya unyonyeshaji Tanzania ikipungua kwa asilimia 1% ambapo
sawa na watoto elfu 20 hawanyonyeshwi.
No comments:
Post a Comment