Rais
Magufuli amemtaka Mfanyabishara Mohamed Dewji (Mo Dewji), kuhakikisha
anajali maslahi ya wafanyakazi wake kama anavyofanya katika Timu ya
mpira wa miguu ya Simba Sports Club ambapo amemsihi kwamba wafanyakazi
hao nao wanastahili kupata maslahi yao.
Ametoa
ombi hilo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and
Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na
mfanyabiashara huyo.
“Mohamed
Dewji ninakupongeza sana katika hili na ninakuomba uwajali wananchi
wanaofanya kazi hapa hasa maslahi yao kwahiyo unapokuwa unaangalia
maslahi ya Simba uangalie pia masilahi ya wafanyakazi wa 21st century
food and packaging,” amesema.
Aidha
ameiataka Kampuni ya Metl Group iliyopo chini ya mfanyabishara huyo
kuachana na utaratibu walionao wa kuagiza ngano kutoka nje ya nchi na
badala yake kuanza kulima ngano nchini kwani kwa kufanya hivyo
itasawadia Watanzania wanaohitaji ajira.
“Ninatoa
wito kwa Kampuni ya Metl Group chini ya Mohamed Dewji, nilipokuwa
ninapewa maelekezo nmeambiwa mahindi yanatoka Tanzania ambayo
yanatengenezwa tani 300 kwa siku lakini ngano inayotengeneza tani 1400
kwa siku inaagizwa kutoka nje hii tuibadilishe,” amesema.
“Katika
maisha yangu nilikua ninafahamu kulikuwa na mashamba makubwa sana ya
ngano kule Manyara lakini sasa hivi hayatumiki na kuna wakati wawekezaji
wakijaribu wanachomewa moto sasa nitoe wito hata kwa Kampuni yako
muanze kulima ngano kwani mtakuwa mmesaidia Watanzania wengi,” amesema.
No comments:
Post a Comment