![]() |
| Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akionesha kitabu cha Mpango mkakati wa kupambana na maradhi ya Homa ya Ini katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar. |
Waziri
wa Afya Hamad Rashid Mohamed katikati akikata utepe kuashiria Uzinduzi
wa Mpango mkakati wa kupambana na maradhi ya Homa ya Ini katika mkutano
na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini
Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla
iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

Msaidizi
Mpango shirikishi Ukimwi,Homa ya Ini,Kifua kikuu na Ukoma Issa Abeid
Mussa akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na
Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake
tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya
Mnazi mmoja Zanzibar.

Muakilishi
wa Shirika la Afya Duniani(WHO)Dk,Ghirmany Andemichael akitoa taarifa
ya WHO katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya
Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia kilele chake tarehe 28
Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja
Zanzibar.

Waziri
wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari
kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo itafikia
kilele chake tarehe 28 Julay 2019 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa
Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
****************
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 26/07/2019.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imeahidi kushirikiana na sekta
mbalimbali za ...ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inafikia lengo la
kuondoa Homa ya Ini Zanzibar ifikapo mwaka 2030.
Hayo
aliyasema Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed huko katika Ukumbi wa
Wizara ya Afya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini
duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Julai 28 ya kila mwaka .
Amesema
Serikali imepanga mikakati kuweza kudhibiti homa hiyo kwa kuwapatia
matibabu ya chanjo wenye mahitaji maalum ikiwemo wauguzi ambao
wanawahudumia wagonjwa mbali mbali ili waweze kujiepusha na maambukizi.
Amesema
ugonjwa wa homa ya ini imeenea sana duniani kote hasa Bara la Afrika na
zaidi kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo Zanzibar
takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha wastani wa watu milioni 257 wanaishi
na maambukizi ya homa ya ini B na milioni 71 ya homa ya ini C duniani
na vile vile watu karibu milioni 1.4 hufa kila mwaka kutokana na
madhara ya maradhi hayo .
Ameeleza
ripoti za utafiti maalum wa kutathmini hali halisi ya homa ya ini bado
haujafanyika Zanzibar ambapo takwimu zinathibitisha uwepo wa
maambukizi ya homa ya ini inaonyesha walioathirika zaidi na ugonjwa huo
ni watu wa makundi maalum (key population )ambao wamefikia asilimia 2-6
kwa homa ya ini B na asilimia 1-25 ya homa ya ini C.
Alifahamisha
miongoni mwa watu waliopimwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa hiyari
katika mwaka 2011 -2016 walionekana kuambukizwa ya homa ya ini B ni
asilimia 2.4 na ini C asilimia 0.4
Waziri
Hamadi amesema anza ya Serikali kuwapa huduma wananchi wake wote bila
ya ubaguzi kwa lengo la kuwanusuru kutokana na madhara pamoja na vifo
vinavyoweza kusababishwa na homa ya ini .
Aidha
alisema Wizara ya Afya imeunda kitengo maalumu cha huduma ya homa hiyo
ili kupanga kuongoza na kusimamia utekelezaji wa huduma ya homa ya ini
katika ngazi ya taifa wilaya vituo vya afya na jamiii
Alieleza
tayari Wizara imeanza kutoa elimu kuhusu homa ya ini katika ngazi zote
za huduma ya afya ili kuengeza uelewa pamoja na kuhamasisha kinga kwa
wafanyakazi ili kutoa ushauri na msaada wa kitaalamu katika mapambano
dhidi ya homa ya ini .
Kauli mbio ya mwaka huu ni WEKEZA KATIKA KUONDOA HOMA YA INI ZANZIBAR .
Mapema
Waziri wa Afya Hamadi Rashid Mohamed alizindua chanjo ya homa ya ini
kwa wafanyakazi wa hospitali ya mnazi mmoja na kuwataka wafanyakazi hao
kujikinga kwa chanjo hiyo
Hata
hivyo aliwataka wauguzi kufuata maadili ya kikazi kwa kutotoa taarifa
za wagonjwa wanaowapatia tiba pale wanapofika hospitalini hapo kwa
matibabu
Alisema
homa hii imeanza kuiathiri jamii hivyo mkakati wa pamoja unahitajika
kwa kuweza kuutokomeza kwa kutumia chanjo na masharti yaliyowekwa
Nae
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk Marijani
Msafiri alisema zoezi la chanjo kwa wafanyakazi ni muhimu kwani maradhi
hutoka kwa mgonjwa kuja kwa muunguzi
Alisema
chanjo zilizopo zitakidhi kwa wafanyakazi wa hospitali ya mnazi mmoja
hivyo aliwataka wauguzi kuendelea na zoezi hilo ili kufikia malengo ya
serikali kwani ugonjwa huu maambukizi yake huwa kama ya virusi
vinavyosababisha ukimwi .


No comments:
Post a Comment