Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaa mbalimbali vya hospitali
vilivyotolewa na Taasisi ya Helping Hand na Taasisi ya Jamii Bora kwa
ajili ya Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya wilayani Ruangwa, kwenye
viwanja vya Zahanati ya Nandagala wilayani humo, Julai 28, 2019.
Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala. Wa
pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Jamii Bora, Yassir Salim. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kitanda ambacho ni moja kati ya vifaa
vingi vya hospitali vilivyotolewa na Taasisi ya Helping Hand kwa ajili
ya Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya wilayani Ruangwa na kukabidhiwa
kwake na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Salum Tahir (kushoto) kwenye
viwanja vya Zahanati ya Nandagala wilayani humo, Julai 28, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisis ya Jamii
Bora, Yassir Salim wakati alipowasili kwenye Zahanati ya Nandagala
wilayani Ruangwa kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vye thamani
ya ya shilingi milioni 250 vilivyotolewa na Taasisi hiyo ikishirikiana
na Taasisi ya Helping Hand. Pia alipokea madirisha ya aluminiam na
milango kwa ajili ya zahanati hiyo pamoja na kompyuta na madaftari kwa
ajili ya shule wilayani humo vyenye tahamani ya shilingi milioni 25
vilivyotolewa na Benki ya NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye
viwanja vya zahanati ya Nandagala Julai 28, 2019. Kulia ni Vicky Bishubo
ambaye ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali katika Benki ya NMB.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salum Tahir (kushoto)
ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Helping Hand kuhusu vifaa mbalimbali
vya hospitali alivyokabidhiw na Taasisi ya hiyo kwa ajili ya hospitali,
zahanati na Vituo vya Afya wilayani Ruangwa. Mahakabidhiano hayo
yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala Julai 28, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya
Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo (wapili kulia) kuhusu
kompyuta na madaftari kwa ajili ya shule wilayani Ruangwa pamoja na
madirisha ya aluminium na milango kwa ajili zahanati ya Nandagala .
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala Julai 28,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya
hospitali kutoka Taasisisi ya Helping Hand vyenye thamani ya sh.
Milioni 250 pamoja na madirisha ya aluminium, milango kwa ajili ya
zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pia kompyuta na madftari kwa
ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya sh.milioni 25
vilivyotolewa na Benki ya NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye
viwanja vya zahanati ya Nandagala, julai 28, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kupokea madirisha ya aluminium na
milango kwa ajili ya zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pia
kompyuta na madftari kwa ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya
sh.milioni 25 vilivyotolewa na NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika
kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala,Julai 28, 2019. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)NA OWM, RWANGWA
*Ni vya shule ya sekondari na zahanati
ya Nandangala
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea
msaada wa vifaa mbalimbali kutoka benki ya NMB vyenye thamani ya sh. milioni 25.
Vifaa hivyo ni fremu 46 za madirisha ya
alminium na vioo vyake, milango 18, mabati 56, misumari na mbao, kompyuta 10,
madaftari 4,050 vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 25/-.
Akipokea msaada huo leo mchana (Jumapili,
Julai 28, 2019) kwenye zahanati ya Nandagala, wilayani Ruangwa mkoani Lindi,
Waziri Mkuu amewashukuru viongozi wa benki hiyo kwa kuamua kuchangia vifaa
hivyo.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nandagala,
Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, amesema mchango uliotolewa
unamaanisha kazi ya kukamilisha jengo la wodi ya wagonjwa na vyumba vya
madaktari ni lazima ifanyike haraka.
“Tunamshukuru Mkurugenzi Mkuu wa NMB kwa
msaada huu mkubwa. Hii maana yake ni kwamba ni lazima tuharakishe kukamilisha
jengohili ili tuanze kutoa huduma kwa wananchi wa Nandagala na wa vijiji vya
jirani,” alisema.
“Tulianza na ujenzi wa zahanati kisha
tukajenga jengo la upasuaji lenye wodi mbili. Moja ya wanaume na nyingine ya
wanawake ambazo kila moja ina uwezo wa kulaza wagonjwa 20 kwa wakati mmoja.”
Jengo hili jipya ambalo tumelianza ujenzi
wake, likikamilika litakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 60. Pia kuna jengo
lenye vyumba vya madaktari, vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia.
Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao
wafikirie uwezekano wa kujenga wodi nyingine na pamoja na jiko ili wagonjwa
watakaokuwa wanalazwa hapo, wapate mahali pa kupikiwa chakula.
Mapema, akitoa taarifa ya
msaada huo, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali katika benki ya NMB, Bi. Vicky
Bishubo alisema kipaumbele cha benki hiyo kila mara ni kutatua changamoto za
afya na elimu kwani sekta hizo ni nguzo kuu ya maendeleo kwa Taifa lolote.
“Vitu hivi (mabati, madirisha ya
aluminium, kompyuta na madaftari) tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu
katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha
jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” alisema.
Alisema kwa mwaka huu, NMB imetenga zaidi
ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo
kusaidia sekta ya afya na elimu. “Mpaka ninavyoongea leo, tayari tumetoa
misaada yenye thamani ya zaidi ya millioni 600 kwa mwaka huu wa 2019 tu,”
alisema.
Akielezea kuhusu programu ya WAJIBU, Bi.
Bishubo alisema hadi sasa wameshawafikia vijana wasiopungua 42,000 katika shule
za msingi na sekondari kwa kuwapa elimu ya fedha na kujifunza kuweka akiba
katika umri mdogo kupitia programu yake ya ‘Jifunze, Jipange na Wajibika’ (WAJIBU).
“NMB imekuwa ikiwawezesha vijana kupata elimu
ya fedha katika shule za msingi na sekondari Tanzania. Elimu hii ya fedha kwa
vijana hutolewa na wafanyakazi wetu wa benki kwenye shule zilizopo karibu na
benki ikilenga kuwafundisha vijana umuhimu wa kuweka akiba na mipango kwa ajili
ya maendeleo yao na kukidhi mahitaji ya muhimu,” alisema.
Kwa
upande wake, Diwani wa Kata ya Nandagala, Bw. Andrew Chikongwe aliishukuru benki
hiyo kwa kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo alisema vimefika kwa wakati muafaka. “Majengo
yalikwishakamilika, yakabakia madirisha na milango, pamoja na vifaatiba, kwa
hiyo sasa hivi tunaweza kuendelea na ujenzi,” alisema.
No comments:
Post a Comment