Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo akitoa maelezo jinsi gani wanavyovuna utomvu kwa baadhi
ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji
vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita
baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli
mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.
Baadhi
ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji
vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita
wakishangaa jinsi miti inavyoweza kutoa mabilioni ya fedha baada ya
kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za
uendeshaji katika shamba hilo
Moja kati ya maeneo ya Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
***
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Watanzania
kuanza kunufaika na zao la miti kutokana na uvunaji wa utomvu kutoka
kwenye miti ya kupandwa iliyopo kwenye Shamba la Sao Hill lililopo
Mufindi mkoani Iringa kwa kuiliingizia taifa zaidi ya shilingi bilioni
mbili kwa kupindi cha miaka miwili ya majaribio.
Hiyo
imebainika wakati wa ziara ya baadhi ya viongozi wa wilaya ya
Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la
Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la
Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika
shamba hilo.
Akitoa
ufafanuzi mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo
alisema kuwa Shamba la Miti Sao Hill wameanziasha mradi mpya wa kuvuna
utomvu ambao umekuwa unatengenezewa gundi kwa ajili ya kutumika kwenye
bidhaa mbalimbali kulinga na mahitaji ya wahusika.
“Tumeanza
kugema utomvu kwenye miti mikubwa kwa kuwa tupo kwenye majaribia lakini
wataalamu wamesema kuwa ukianza kugema utomvu mti ukiwa na umri mdogo
basi utagemwa kwa muda mrefu na kuleta faida kwa wananchi na taifa kwa
ujumla, na kumbukeni kuwa hapa mti haukatwe unaendelea kustawi tu”
alisema Mbwambo
Mbwambo
alisema kuwa takwimu za dunia zinaonyesha kuwa inawezekana utomvu ukawa
unalipa zaidi ya zao la miti hivyo utafiti ukimalizika yawezekana
wakulima wa miti wakahamia kwenye uvumaji wa utomvu.
“Kwa
takwimu hizo sio muda faida kubwa itakuja kwa wananchi na serikali kwa
ujumla maana inaonyesha dhahili kuwa utomvu unalipa sana kuliko mbao
hiyo watafiti waliopo hapa katika shamba la Sao Hill ukizaa matunda basi
utahamia kwa wakulima wa miti” alisema Mbwambo
Mbwambo
alisema kuwa miti milioni tatu kila mwaka ndio inatumika katika uvunaji
wa utomvu na hakuna eneo maalum ambao limetengwa kwa ajili ya kuvuna
bali wametoa maeneo ambayo yanamiti ambayo inatarajiwa kuvunwa baada ya
miaka miwili ijayo
“Shamba
hili la Sao Hill ni kubwa sana linakaribia kuwa na hekta laki moja na
elfu hamsini na nne hivyo sio rahisi kufanya majaribio shamba lote hiyo
tumetoa eneo ambalo miti yake inatarajiwa kuvunwa baada ya miaka miwili”
alisema Mbwambo
Mbwambo
alisema kuwa soko la utomvu duniani kwa sasa linategemee kutoka nchi
China hivyo soko lipo huko na kampuni ya AATY Limited ya kichini
inavyovuna hapa katika shamba la Sao Hill na ni kampuni kubwa kuliko
zote dunia za uvunaji wa utomvu duniani.
Akizungumza
kwenye eneo la tukio mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe.
Eng. Mtemi Msafiri alisema kuwa wamejifunza kitu kipya ambacho
hawakuwahi kukifikiria katika maisha yao kuwa uvunaji au ugemaji wa
utomvu unalipa kwa namna hiyo.
“Navyo
sema kuwa sasa tumegundua dhahabu ya kijani namaanisha hivi,utomvu
unaigiza fedha nyingi tumeana hapa mkurugenzi katueleza hivyo ni lazima
tuchukue swala hili kwa umuhimu stahili ili hata kweli kwetu Chato
tutalifanya kwa umakini mno” alisema Msafiri

No comments:
Post a Comment