Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa amedai
uamuzi uliofanywa na Spika wa Bunge Job Ndugai wa kumvua Ubunge
aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu uko sawa, kwani yeye
alishawahi kuwavua Wabunge zaidi ya 50 katika kipindi chake, kwa kosa la
utoro ndani ya Bunge.
"Uzoefu
wangu mimi katika hili Spika yuko sawa kabisa, kwa sababu hata mimi
mwenyewe nilishawavua Wabunge wengi kipindi cha uongozi wangu
nawashangaa sana wanaohoji hatua hiyo, ni jambo la Kikatiba lililofanywa
na Spika Ndugai" amesema Msekwa
"Mimi
mwenyewe niliwavua wengi tu na wala sio mmoja, Wabunge wa Zanzibar
walikiuka kifungu cha Katiba alichokinukuu Spika Ndugai, tena walikuwa
kama 50 hivi wote nikawavua Ubunge na uchaguzi ulifanyikla tena."
ameongeza Msekwa
"Inawezekana
watu wakasema Tundu Lissu nchi nzima inajua kuwa anaumwa, lakini katiba
haisemi kuwa lazima usikilize kutoka magazetini au mitandaoni inatakiwa
Mbunge aandike barua." amesema Pius Msekwa
June
28 katika vikao vya kujadili miswada mbalimbali ya kisheria kwa ajili
ya mwaka mpya wa fedha Spika Job Ndugai alitangaza kuwa jimbo la Singida
Mashariki liko wazi kufuatia Mbunge wake kutotoa taarifa kuwa yuko
wapi.
No comments:
Post a Comment