![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker, Waziri wa Nishati Medard Kalemani pamoja na viongozi wengine akisikiliza namna mradi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji utakavyokuwa ukifanya kazi mara baada ya kukamilika. |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt.
Mohamed Shaker wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi
wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji
katikati ya Morogoro na Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker mara baada ya
kuweka Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115
katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifurahia pamoja na viongozi wengine mara baada ya tukio hilo la
uwekaji wa Jiwe la Msingi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri
wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker, Waziri wa Nishati Medard
Kalemani pamoja na viongozi wengine akisikiliza namna mradi wa Kuzalisha
umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji utakavyokuwa ukifanya
kazi mara baada ya kukamilika.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia michoro ya ujenzi huo mkubwa wa kufua umeme.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa
Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker wakati
wakielekea kwenda kuweka jiwe hilo la msingi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo itakayotumika katika mradi
huo mkubwa wa kufua umeme.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia eneo la bonde katika mto Rufiji mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la mradi huo wa umeme.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi.
Eneo la mto Rufiji ambalo litatumika katika ujenzi huo wa kufua umeme kama linavyoonekana. PICHA NA IKULURAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Julai 26,
2019 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa ...kuzalisha umeme wa Megawati
2115 katika mto rufiji mkoani Pwani ambao utakamilika Juni 2022.
Sherehe
za uwekaji jiwe hilo la msingi zimefanyika kandokando ya eneo ambalo bwawa
litajengwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson, Waziri wa Nishati wa Misri Mhe.Dkt. Mohammed Shaker, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani,
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangallah, Manaibu Waziri,
viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama na viongoze wengine wa ngazi
mbalimbali.
Ujenzi
wa bwawa hilo utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 6.5 na
litakuwa bwawa kubwa kabisa katika ukanda wa Afrika Mashariki na la nne kwa
ukubwa barani Afrika.
Katika
hotuba yake, Mhe. Rais alisema kwa kutambua mapenzi na maono ya Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amependekeza bwawa hilo lipewe jina la Bwawa
la Nyerere.
Rais
Magufuli ameipongeza Wizara ya Nishati kwa utekelezaji wa mradi huo na ameeleza
kwamba Serikali imechukua hatua ya ujenzi wa bwawa hilo ili kuongeza uzalishaji
wa nishati ya umeme kutoka Megawati 1,601 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia
Megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Aidha
Mhe. Rais amewataka wakandarasi (Arab Contractors na Elsewedy) kutoka nchini
Misri kabla ya Juni 2022 hasa ikizingatiwa hakuna tatizo la fedha ili
Watanzania waanze kunufaika mapema.













No comments:
Post a Comment