Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho
kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida wakati wa
warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za
Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS)
iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (EAC-
PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa kitengo cha maendeleo ya sekta binafsi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Diana Makule akiwasilisha mada ya mtazamo wa jumla wa PSDS 2006 na
matokeo ya utekelezaji wake wakati wa warsha iliyoandaliwa na ESRF
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya tabia nchi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha
Ngalowera akiwasilisha mada kuhusu uchakataji wa mazao ya kilimo katika
mradi wa PSDS 2006 kwa kuangalia vifungu vinavyohusiana na tabia nchi
kwenye warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa warsha, Meneja Ufuatiliaji na Tathmini , Kituo cha
Taasisi ya Maendeleo Endelevu (CSDI), Dk Isaack Nguliki akizungumzia
biashara kuchagiza uchakataji wa mazao ya kilimo kwa kuangalia vifungu
vinavyohusiana na tabia nchi katika PSDS kwenye warsha iliyoandaliwa na
ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Bi. Rehema Mbugu kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF)akiongoza majadiliano ya mtazamo wa jumla wa PSDS 2006 na matokeo
ya utekelezaji wake wakati wa warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakishiriki majadiliano wakati wa warsha ya kitaifa ya
utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki
unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala
Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango
akisisitiza jambo wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati
wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta
binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar
es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akifafanua jambo wakati wa
warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za
Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS)
iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
**
Wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imejikita katika kutaka
kuendeleza mkakati wa sekta binafsi (PSDS) 2018-2022, wenye lengo la
kuweka mazingira mazuri ya biashara yatakayochochea ushindani ndani ya
sekta binafsi kwa kuongeza uwekezaji, tija na biashara, Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imekutanisha wadau kuangalia namna
ya kuboresha mkakati huo.
Katika warsha hiyo wadau walizungumzia na kuainisha mambo mbalimbali
yenye lengo la kuuwezesha Mkakati huo kutoa mchango wenye uelewa wa
mabadiliko ya tabia nchi, uzalishaji wenye msukumo wa kibiashara na
uchakataji wa bidhaa za kilimo.
Dk. Tausi Kida Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), akifungua warsha hiyo mwishoni mwa wiki alitaka
washiriki kuwa makini ili kuweza kuona namna gani wanaweza kuimarisha
mkakati huo.
Akishawishi umakini katika warsha hiyo ya kitaifa ya utekelezaji wa
mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango
wa sekta binafsi (EAC- PSDS), alisema bila umakini mchango wa mkakati
huo hautaonekana.
Katika warsha hiyo wadau walizungumzia upenyo wa maendeleo endelevu katika uchakataji wa bidhaa za kilimo.
Warsha hiyo ikiwa ni sehemu ya awamu ya pili ya mradi wa kuendeleza
kilimo katika nchi za Afrika mashariki unaoangalia mabadiliko ya tabia
nchi na mahusiano ya kibiashara katika nchi hizo- (PACT EAC2). Mradi huo
umekuwa ukiendeshwa na ESRF kwa kushirikiana na CUTS International
yenye makao makuu yake mjini Geneva Uswisi.
Mkurugenzi huyo wa ESRF alisema kwamba toka mwaka 2015 mradi umekuwa
ukifanya majadiliano ya kina kwa sekta mbalimbali ambazo nyingi ni
mtambuka ili wadau wengi wawe wanajua kwa pamoja mabadiliko ya tabia
nchi, mahusiano yao na uzalishaji, biashara, usalama wa chakula na
viwanda vya kuchakata bidhaa za kilimo.
Kwa mujibu wa Dk Tausi warsha hiyo ilikuwa na lengo la kuwapa nafasi
wadau wote kuangalia njia bora zaidi ya kuwezesha uchakataji endelevu wa
viwanda vya bidhaa za kilimo ili kuvipa thamani kupitia sekta binafsi.
Mkurugenzi huyo aliwataka washiriki kujadili kwa kina mchango wa sekta
binafsi katika kuchagiza uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, na
uendelezaji wa kilimo biashara na usalama wa chakula katika ukanda huu
wa Afrika Mashariki.
“Kutokana na ukweli huo napenda mazungumzo yetu ya leo yajikite zaidi
katika kufanikisha mkakati wa sekta binafsi kuhusu maendeleo (PSDS)
2018-2022 kuhusu wajibu wake kuendeleza uchakataji wa bidhaa za kilimo
endelevu utakaozingatia mabadiliko ya tabia nchi biashara na usalama wa
chakula.” alisema Dk Tausi.
Katika warsha hiyo ambapo mada mbili ziliwasilishwa moja ikizingatia
mabadiliko ya siasa na sheria nchini na mazingira ya sasa kuhusiana na
mkakati huo wa kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi na dhana ya uendelezaji
wa kilimo biashara katika uhusiano na mabadiliko ya tabia nchi na
nyingine.
Mada hizo zimetolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na
Ofisi ya Waziri Mkuu,wakiangalia PSDS ilivyowezeshwa kusaidia sekta
binafsi kuchochea uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, kilimo biashara na
uchakataji wa bidhaa za kilimo na usalama wa chakula.
Mada hizo ziliwasilishwa na Diana Makule wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Martha Ngalowera wa Ofisi ya Makamu wa Rais.
No comments:
Post a Comment