Afisa wa TCRA Kanda ya Kaskazini Bw. Oswald Octavian (katikati) |
Abubakar
Karinga(kushoto), Afisa Usajili Mkoa-NIDA Kilimanjaro, akitoa maelezo
kwa watu waliofika kuhudumiwa katika "Mnadakw amnada" leo Juni 28, 2019.
Dorice A.Mhimbira (kushoto), Afisa Masoko TCRA, akimsikiliza mkazi wa Manispaa ya Moshi, aliyefika kwenye zoezi la "Mnada kwa mnada" kwenye stendi kuu ya Manispaa ya Mji wa Moshi Juni 28, 2019 ili kuhudumiwa.
Afisa wa NIDA (kushoto), akiwahudumia wananchi
Watoa huduma ya Mtandao wa simu za mikonini Tigo, wakisajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole biometria
Watoa huduma ya mitandao ya simu kutoka Airtel nao walikuwepo.
Watoa huduma ya mitandao ya simu za mikononi kutoka Vodacom nao walikuwepo kuhudumia wananchi.
Maafisa wq aNIDA wakiwa na zana zao tayari kutoa huduma.
Afisa wa NIDA (kulia), akiwahudumia wananchi
Calistus
Mhode (wapili kushoto), Mkaguzi Msaidizi wa Police Cyber Crime,
akimuelimisha mwananachi huyu kuhusu athari za makossa ya kimtandao
wakati alipofika kuhudumiwa kwenye mnada kwa mnada
NA
K-VIS BLOG, MOSHI
MAMIA
ya wakazi wa Manispaa ya Mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro wamefurika kwenye
zoezi la “Mnada Kwa Mnada” la kuwapelekea huduma wananchi huko waliko
ili kusajili laini za simu kwa mfumo mpya wa kutumia alama za vidole yaani
kitaalamu Biometria.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwenye zoezi hilo ambalo linasimamiwa na TCRA, pia linahusisha taasisi
nyingine za Umma na watoa huduma za mitandao ya simu ili kuwarahisishia
wananchi kupata huduma mahala pamoja (One Stop Centre).
Taarifa hiyo imezitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na TCRA yenyewe, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), Idara ya Uhamiaji, Kitengo cha polisi kinachosimamia makosa ya
kimtandao yaani (Police Cyber Crime
Department) na watoa huduma za mitandao ya simu za mikononi.
“Taratibu
za kujisajili na mfumo huu mpya wa kutumia alama za vidole Biometria zinamtaka mtu anayetajka kujisajili sharti awe na
kitambulisho cha taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa,” Taarifa imesema na kuongeza…
Ili
uwe na kitambulisho cha Taifa, ni lazima taarifa zako za uraia au ukazi zithibitishwe
na Idara ya Uhamiaji ambapo zoezi hilo likikamilika, NIDA itatoa namba ya
Kitambulisho cha taifa ambayo mwananachi ataiutumia ili kusajili laini yake kwa
watoa huduma za mitandao ya simu za mikononi ambao ni TTCL, AIRTEL, TIGO,
VODACOM, HALOTEL na ZANTEL.
No comments:
Post a Comment