Pages

Saturday, June 29, 2019

India yafanyia majaribio kombora lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia


Serikali ya India imelifanyia majaribio kombora la balestiki linaloitwa Prithvi II lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia.

Majaribio ya kombora hilo la kutoka ardhini kuelekea angani la Prithvi II lilibebwa na trela la kubebea mizigo kwa umbali wa kilometa 350 kupitia maeneo ya mji wa Chandrapur wa jimbo la Odisha kusini mwa India.

 Kwa mujibu wa habari hiyo, kombora hilo la balestiki sambamba na kubadili mwelekeo, linaweza pia kuzuia utendajikazi wa mfumo wa makombora. 

Aidha kombora hilo linaweza kubeba vichwa vya mabomu ya kivita na nyuklia kutoka uzito wa kilogramu 500 hadi kilogramu 1000. 

Inafaa kuashiria kuwa, India na Pakistan zimekuwa katika ushindani mkubwa wa kumiliki silaha za nyuklia ambapo kila moja imekuwa ikifanya majaribio ya makombora tofauti yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia.

Katika uwanja huo mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu Meja Jenerali Asif Ghafoor, Msemaji wa jeshi la Pakistan alitangaza kuwa, endapo kutatokea vita baina ya India na Pakistan, basi mwanzoni tu mwa vita hivyo, Pakistan itaisambaratisha miji ya Mumbai na New Delhi na kuisawazisha na uso wa ardhi. 

Ghafoor aliyeyasema hayo baada ya kujiri mapigano mafupi kati ya nchi mbili alisisitiza kwamba, jeshi la nchi hiyo likiwa na silaha nzito za aina tofauti limejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuishambulia Kashmir iliyoko katika udhibiti wa India.

No comments:

Post a Comment