Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenzwa na wajane wakati
alipotembekea banda la Mtandao wa wajane Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya
Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Na
Christian Gaya gayagmc@yahoo.com
Majira
28.Juni.2019
Siku ya wajane duniani kila mwaka hufanyika
mwezi Juni 23. Ambapo kwa mwaka huu maandamano ya kusheherekea siku hii ya wajane
Duniani yalifanyika jijini Dodoma.
Wajane na wagane pamoja na watoto wao wana
wajibu wa kujua mafao ya urithi yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii kama
haki yao kama aliyekuwa...
wanamtegemea alikuwa mwanachama hai wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
wanamtegemea alikuwa mwanachama hai wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Wanatakiwa kujua sifa zinazotakiwa ili kupata
mafao hayo ya urithi, mafao yanayotolewa, mgawanyo wa pensheni hizo za urithi,
pamoja na viambatanisho vinavyotakiwa wakati wa kufungua madai yao.
Baada ya kuijua, vile vile ni wajibu wao
kuhakikisha ya kuwa wanafuatilia kwa kutembelea ofisi za mifuko ya pensheni ya
hifadhi ya jamii. Wategemezi wanatakiwa kufanya hivyo bila kuchoka au kukata
tamaa. Utafiti unaonesha ya kuwa idadi kubwa ya wajane au wagane na watoto wao
hawatambui au hawajui haki zao za mafao ya urithi. Hivyo wengi wao hawajui ofisi za hifadhi ya jamii zilipo na
hata namna ya kufuatilia hizo haki.
Mara
nyingi changamoto kubwa wanayoipigia kelele wajane wengi nchini ni hali ya
uchumi kuporomoka pindi wakiondokewa na wenza wao, hivyo tatizo hilo pia
huongeza idadi ya watoto yatima mitaani. Baadhi ya mila za
makabila fulani hapa nchini zinazofanyika katika jamii zetu huwa
zinawagandamiza na kuwanyanyasa wajane, wagane na watoto wao.
Hata kama yatima wameachwa wakiwa watu wazima,
wanaweza wasifahamu kwamba wanapaswa kurithi kiasi gani cha mali ya marehemu
baba yao. Tatizo kama hili linaweza kujitokeza iwapo marehemu alikuwa hajagawa
urithi kwa wanawe, au hakuacha wosia wowote.
Vile
vile kama mama mzazi wa watoto bado yupo hai, kunaweza kutokea mgongano kati ya
watoto na mama yao, wakati wa kugawana mali iliyoachwa na marehemu. Lengo la
kutunga sheria inayosimamia maswala ya urithi ni kuepusha migongano kwa
kuhakikisha kuwa haki ya kila anayestahili kurithi inalindwa
Ili
kukwepa changamoto hizo watanzania wanatakiwa kujiunga kwa mpango wa hiari na
mpango lazima yanayoendeshwa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini na hii
haijarishi kama anafanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi au sekta iliyo rasmi na
hata binafsi.
Kuwepo
kwa mifuko hii ya hifadhi ya jamii kunaweza kuwa msaada mkubwa kwa wajane au
wagane na watoto wao pindi mwanachama mwanamke au mwanamme wa mfuko wa hifadhi
ya jamii marehemu anapofariki kuwa ndio kimbilio la watu wengi wa kundi kama
mwanaume au mwanawake alikuwa mwanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii
Ambapo
inaweza kuwasaidia wajane au wagane hata kuanzisha miradi mbalimbali ya kuweza
kuinua kimaisha ikiwemo ya kufanya
biashara ndogondogo za ujasiriamali, kama tulivyojionea mwaka huu jijini Dodoma
wajane wengi wakionesha bidhaa za aina mbalimbali wakati wa kusherekea siku ya
wajane duniani.
Inataja
wazi ya kuwa mafao ya urithi hulipwa kwa warithi wa mwanachama wa ZSSF
aliyefariki dunia akiwa bado yupo katika ajira na akiwa bado hajalipwa mafao ya
uzeeni au ya ulemavu. Mafao ya urithi ni ya mkupuo tu na hulipwa warithi kwa
mujibu wa sheria za mirathi ya imani ya wahusika
Mara
baada ya kukamilika taratibu za hesabu, malipo kwa warithi hupitia Kamisheni ya
Wakfu na mali ya amana kwa ajili ya warithi wa Imani ya Kiislamu na malipo
mengine hufanyika kupitia ofisi ya Mrajisi Mkuu wa Serikali kwa ajili ya
warithi wa imani ya Kikristo na nyenginezo.
Sheria
hii ya ZSSF inasema ili mwanachama aweze kupata mafao ya urithi, anahitajika
kuwasilisha vielelezo kama vile cheti cha uthibitisho wa kifo au kibali cha
mazishi, barua ya mwajiri yenye kuthibitisha kufariki kwa Mwajiri husika na
kuwaombea mafao warithi wake.
Na
vielelezo vingine ni barua binafsi ya warithi au msimamizi wa mirathi ya kuomba
mafao. kadi ya uanachama ya ZSSF ya marehemu, fomu ya maombi SSF 11 ambayo
hupatikanwa na kujazwa mbele ya ofisa mafao katika ofisi za ZSSF.
Hapa
itambuliwe ya kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kutoa mafao ya urithi kwa
yatima na wajane wanaotambuliwa kisheria na kwa utaratibu unaoeleweka ni njia
mojawapo ya kupiga vita mila potofu kama za kurithi na kutakasa wajane na
watoto wao, ambapo mara nyingi tumeone wajane na yatima kunyanyaswa kijinsia.
Hivyo
kwa upande wa utaratibu na sheria za hifadhi ya jamii nchini zinazohusu mafao
urithi utafiti unaonesha ya kuwa zinaweza kuwa rafiki kwa wajane, wagane na
watoto wao.
ZSSF ilianzishwa
mwaka 1998 katika awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dk. Salmin Amour Juma
kwa lengo la kutatua changamoto mbili kuu. Awali kuisaidia Serikali katika
kurahisisha upatikanaji wa mafao kwa watumishi wake kwa wakati huo. Lakini pia
kuharakisha upatikanaji wa malipo hayo kwa haraka na kwa wakati muafaka.
Mfuko wa ZSSF unatekeleza
majukumu yake kutokana na sheria nambari 2 ya mwaka 2005, Sheria ambayo
ilifanyiwa marekebisho mwaka 2016 kwa lengo la kuufanya Mfuko wa ZSSF kuwa
endelevu na kupanua wigo kwa kuwajumuisha katika wigo wa hifadhi ya jamii walio
katika sekta isiyo rasmi kwa maana waliojiajiri wenyewe ambapo kwa sasa wana
fursa ya kujichangia kwa hiari.
Kwa mujibu wa sheria hiyo,
Mfuko unalipa kwa wanachama wake mafao manne katika ya mafao matano yanayotajwa
kwa mujibu wa Sheria.
Mafao yanayolipwa ni mafao ya
uzeeni yakijumuisha pensheni na kiinua mgongo kwa wastaafu, mafao ya urithi,
mafao ya ulemavu na mafao uzazi kwa wanachama wanawake.
“Aidha fao la matibabu kwa sasa linafanyiwa tathmini na wataalamu
ambalo linategemewa kuwa litakuwa fao la tano kwa mujibu wa sheria na mara
mipango hiyo itakapokamilika, mfuko wa ZSSF ukishirikiana na Serikali utatoa
maelekezo rasmi juu ya fao hilo la matibabu.” Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF
Sabra Issa Machano anafafanua zaidi.
No comments:
Post a Comment