Pages

Monday, May 27, 2019

Zijue faida za parachichi katika kulinda afya yako

Parachichi ni tunda lenye mbegu moja na virutubisho vingi sana, na tunda hili hulimwa sehemu mbalimbali duniani, ila ni tunda linalolimwa kwa wingi, Mexico na Amerika ya kusini na baadae kusambaa sehemu nyingine duniani ikiwemo Tanzania. Parachichi ina virutubisho vingi vinavyojulikana kama ”nutrient dense fruit” vikiwa vimebeba kiwango kikubwa cha virutubisho vya protini, mafuta, vitamin, wanga na madini mbalimbali.
Zifuatazo ni faida za kiafya za maparachichi.
Hukuweka katika hali nzuri (mood) kwani baadhi ya tafiti zimeeleza kuwa watu wenye msongo wa mawazo huwa na upungufu mkubwa wa madini ya Potasiamu na parachichi ni tunda lenye madini ya potasiamu hivyo basi tunda hili linaweza kukuweka katika hali nzuri
Husaidia kupunguza mifupa kulainika, Vitamini K inayopatikana kwenye parachichi husaidia unyonywaji wa madini ya kalsiamu ambayo hujenga mifupa na kuwa imara. Ulaji wa parachichi kila siku au mara kwa mara humpa mtu madini ya kutosha ya Vitamin k. Parachichi moja lina kiasi cha asilimia 50 ya mahitaji ya vitamin K kwa siku.
Huboresha afya ya nywele na ngozi, na hii ndiyo sababu parachichi hutumika kutengeneza mafuta ya nywele na ya ngozi kutokana na kusheheni kwa vitamin E ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya nywele na ngozi zetu.
Huboresha afya ya ubongo, madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi kwa zaidi ya asilimia 19 yana nafasi kubwa sana katika kuufanya ubongo ufanye kazi vyema.
Huongeza nguvu za mwili kutokana na kumiliki kiwango kikubwa cha virutubisho vya wanga, protini na mafuta.
Hupunguza lehemu mwilini ( Cholesterol), baadhi ya tafiti zilizofanyika zinaonesha ulaji wa mlo wenye maparachichi kwa wingi kila siku unasaidia kupunguza lehemu mbaya mwilini (LDL Cholesterol) na kuongeza lehemu nzuri , HDL Cholesterol). Pia matumizi ya parachichi moja kila siku yanasaidia kupunguza lehemu hizi kwa watu wenye uzito mkubwa.

No comments:

Post a Comment