Mratibu
wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa
akizungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) linalotarajia kufanyika
katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Kulia ni Mwenyekiti wa GAWE,
James Ogondick na Ofisa Utetezi TEN/MET, Bw. David Sizya (kushoto)
|
Na Joachim Mushi
MTANDAO
wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana uliwasimamisha waandishi wa habari
mbalimbali kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano nao, ikiwa ni ishara
ya kumkumbuka Marehemu Dk. Reginald Mengi Mwenyekiti Mtendaji wa
Makampuni ya IPP ambaye amefariki dunia.
Akizungumza
kabla ya tukio hilo, Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga
alisema Marehemu Mengi alikuwa mmoja wa wadau wa elimu na amefanya mambo
mengi kuchangia mafanikio ya sekta hiyo hivyo wanakila sababu ya
kumkumbuka.
"TEN/MET
imeguswa na msiba wa Marehemu Dk. Mengi kwa kuwa alikuwa mdau mzuri
katika kuchangia elimu, amefanya mambo mengi kuchangia na kusaidia
wahitaji katika elimu...naomba tusimame kwa dakika moja kumkumbuka,"
aliwaambia wanahabari.
Jana TEN/MET ilikutana na waandishi wa habari mbalimbali jijini Dar es Salam
kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni.
Mratibu
wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Wayoga akizungumzia maadhimisho hayo alisema
mwaka huu yataanza Mei 6 hadi 10, 2019 katika Viwanja vya Shule ya
Msingi Chanika, huku yakiambatana na mikutano vijiji mbalimbali kwa
madhumuni ya kuhamasisha wanajamii kuhusu ushiriki wa pamoja na serikali
katika kuboresha elimu iliyojumishi na endelevu.
"Tarehe
10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na
mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati
ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu
Bora, Haki Yangu”.
Aidha
alisema maadhimisho ya juma la elimu yatazinduliwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh.
Suleman Jafo mkoani Tanga yatakayofanyika Wilayani Handeni.
No comments:
Post a Comment