Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, kilichotokea huku Dubai Falme za Kiarabu usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2019. Katika ujumbe wake mfupi wa Tweeter, Rais ameandika "Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo ktk kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara."
Dkt. Reginald Abraham Mengi alizaliwa Wilayani Machame Mkoani Kilimanjaro ambapo mara nyingi alikaririwa akisema amezaliwa kwenye familia masikini akichangia chumba anacholalal na mifugo mingine kama mbuzi.
Lakini pamoja na kuwa kwenye mazingira kama hayo, Dkt. Mengi
hakukata tama, ndoto yake ya kufanikiwa kimaisha ilisukuma kusoma kwa bidi. Dkt. Mengi alisomea masuala ya uhasibu nchini Uingereza na baada ya kumaliza masomo yake alirejea nyumbani mnamo mwaka 1971 na kuajiriwa na Kampuni ya Uhasibu na Ukaguzi wa Mahesabu ya Coopers & Lybrand Tanzania (kwa sasa inajulikana kama PriceWaterHouseCoopers)
hadi Septemba 1989 na katika kipindi hicho alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Kiongozi mwenza.
Mnamo Oktoba 1989 Dtk. Mengi aliondoka Coopers & Lybrand Tanzania na kujielekeza kwenye biashara zake binafsi na kuanzisha IPP Limited, ambayo ikuja kuwa kampuni kubwa kabisa ya kibinafsi nchini Tanzania.
Biashara ambazo Watanzania wa kawaida walizifahamu, ni pamoja na
kumiliki vyombo vya habari mashuhuri kabisa hapa nchini ITV/Radio One, Kampuni
ya magazeti ya The Guardian Limited, Kampuni ya kuzalisha vinywaji baridi ya Bonite, lakini pia Dkt. Mengi chini ya kampuni yake ya IPP
alikuwa akifanya biashara mbalimbali na hivi karibuni alisaini kandarasi ya
kuanzisha kiwanda cha kutengeneza magari hapa hapa nchini, lakni pia kiwanda
cha kutengeneza madawa ya binadamu na vingine vingi.
Dkt. Mengi licha ya kushughulika na biashara zake, lakini pia alipenda sana uhifadhi wa mazingira na hilo utalithibitisha ukifika nyumbani kwake Kinondoni na pengine kutokana na sababu hiyo ya kuwa mpenzi wa kuhifadhi mazingira, Serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa, ilimteua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira (NEMC).
Jamii itamkumbuka Dkt. Mengi kutokana na moyo wake wa huruma na upendo, alisaidia makundi mbalimbali ya kijamii kama vile watu wenye ulemavu, ambapo kila mwaka alijumuika nao kwa chakula cha mchana na kubadilishana nao mawazo na lengo kuu likiwa ni kuwashajihisha kutokata tamaa kutokana na ulemavu wao bali wajione kuwa wanaweza kufanya jambo lolote kama wanavyofanya watu wengine.
Makundi mengine ambayo hayatomsahau Dkt. Mengi kutokana na mchango wake wa hali na mali ni pamoja na taasisi za kidini (Waislamu na Wakristo), akina mama, vijana na Wazee lakini pia hata mtu mmoja mmoja, wakiwemo watoto wa mitaani.
Dkt. Mengi alipewa tuzo mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali ukiwemo ubalozi wa Marekani ambao ulimtunuku tuzo ya Martin Luther king kwa uchache.

No comments:
Post a Comment