Pages

Saturday, May 4, 2019

NAIBU SPIKA MH. TULIA ACKSON AONGOZA MBIO ZA TULIA MARATHON 2019 JIJINI MBEYA LEO


01
Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia Ackson akimaliza mbio za kilomita 5 huku akiwa ameongozana Mabalozi wa Tulia Ackson Marathon  Babu Tale kushoto Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz na Msanii Izo Busness  huku akishangiliwa.
Mbio za (Tulia  Marathon 2019) zinafanyika jijini Mbeya zikianzia kwenye uwanja wa Sokoine na kumalizikia uwanjani hapo ambapo kumefanyika mbio za kilomita 42, Kilomita 21, Kilomita 5 na  Kilomita 2 , Mbio hizo zimeshirikisha wanariadha kutoka Kenya na hapa nchini.
1
Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia Ackson akishiriki  mbio za kilomita 5 na Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Mh. William Ntinika pamoja na baadhi ya wabunge.
02
Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia Ackson akivishwa nishani mara baada ya kumaliza mbio za kilomita .
3
Baadhi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pia wameshiriki katika mbio hizo za (Tulia Marathon 2019).
5
Baadhi ya viongozi mbalimbali walioshiriki katika mbio hizo wakijiandaa kuanza mbio hizo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
6
Mbunge wa jimbo la Mbarali Mh. Haroun Pre Mohamed akimaliza mbio za Tulia Ackson 2019  kilomita 5 kwenye uwanja wa Sokoine zilizofanyika leo jijini Mbeya
7
Mbunge wa jimbo la Mbarali Mh. Haroun Pre Mohamed akivishwa nishani mara baada ya kumaliza mbio za Tulia Ackson 2019  kilomita 5 kwenye uwanja wa Sokoine zilizofanyika leo jijini Mbeya
8
Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio za (Tulia Marathon 2019) Kilomita 5
9
Mbunge wa jimbo la Mbinga Mh. Sixtus Mapunda na Cosato Chami wa jimbo la Mafinga wakimalizia mbio za (Tulia Marathon  2019) Kilomita 5.
10
Na hawa nao walishiriki mbio za kilomita 5
11
Mbunge wa jimbo la Mbinga Mh. Sixtus Mapunda na Cosato Chami wa jimbo la Mafinga wakijiandaa na mbio hizo.
12
Rais wa Chama cha Riadha na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka na Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia Ackson wakijiandaa kwa mbio hizo kulia ni Mbunge wa vitimaalu CCM mh. Vick Kamata.
13
Naibu Spika wa Bunge Mh. Tulia Ackson na Rais wa Chama cha Riadha RT Mh. Anthony Mtaka wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge.
14
Viongozi mbalimbali na wabunge wakijiandaa kwa mbio hizo.

No comments:

Post a Comment