Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Makao Makuu ya Bunge la Afrika,Midrand,Johanesburg,Afrika Kusini.
Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Roger Nkodo Dang kutoka nchi ya Cameroon akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini.
Kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiandika dondoo muhimu wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini.
Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiendelea na mkutano.
Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu waliofariki dunia kutokana na majanga yaliyotokea katika baadhi ya nchi za Afrika yakiwemo mafuriko na Kimbunga Keneth.
Mkutano ukiendelea.Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blogKamati ya uongozi ya Bunge la Afrika ‘The Pan African Parliament Bureau’ imekutana na Mabalozi ‘Ambassadors’ wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini kujadili masuala kadha wa kadha kuhusu bara la Afrika.
Mkutano huo ukiongozwa na Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Roger Nkodo Dang kutoka Cameroon, umefanyika
leo Ijumaa Mei 3,2019 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Bunge la Afrika
kama sehemu ya mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge la Tano
la Bunge la Afrika jijini Johannesburg Afrika Kusini.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo wa Mabalozi wa Afrika walioidhinishwa na Jamhuri
ya Afrika Kusini, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa
Stephen Masele ambaye ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu
Waziri wa zamani nchini Tanzania alisema Bunge la Afrika litajadiliana
na kutoa Azimio juu ya tabia ya Xenophobic nchini Afrika Kusini.
“Suala
hili linapaswa kuchukuliwa kwa umakini, kuna vitendo vya uhalifu
vinavyofanywa na vikundi tofauti kutoka nje inaonekana kama Afrika
Kusini haitaki wageni katika nchi yao… La hasha lakini kwa undani kuna
matendo ya uharifu kwa kivuli cha Xenophobia”,alisema Mhe. Masele.
“Ninafurahi
na kuhamasishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini
ili kukabiliana na mambo yote ya uhalifu.Tutakuwa makini sana wakati
tunajadiliana jambo hili kwa sababu hatutaki kuingilia kati mambo ya
ndani ya Afrika Kusini au kuingilia kati vyombo vya usalama kutekeleza
majukumu yao”,aliongeza.
Masele aliomba mamlaka ya Afrika Kusini kushughulikia suala la tabia ya Xenophobic katika Afrika kwani haikubaliki.
“Sisi
kama Wabunge wa Afrika tunatarajia kuona hatua kali zikichukuliwa dhidi
ya waharifu wote, wanaharibu sifa nzuri ya Afrika Kusini na Afrika.
Bunge la Afrika litapaza sauti na kukemea suala hili..Vikwazo vya hali
yoyote dhidi ya watu binafsi au nchi huumiza watu wasiokuwa na hatia
hususani wanawake na watoto na huzuia jitihada za maendeleo za watu wetu
na nchi ambazo zina vikwazo”,aliongeza.
Kikao cha Pili cha kawaida
cha Bunge la Tano la Afrika kinatarajiwa kuanza mnamo Mei 6, 2019 huko
Midrand – jijini Johannesburg Afrika Kusini.
Pamoja na mambo mengine , watajadiliana juu ya Kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu “Mwaka wa Wakimbizi na Watu Waliopotea”,ambapo pia Bunge la Afrika litajadili Suluhisho la Kudumu juu ya tatizo la wakimbizi barani Afrika.
Hali
kadhalika Bunge hilo, litajadili taarifa juu ya amani na usalama katika
bara la Afrika ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hivi karibuni na hali ya
kisiasa Libya, Sudan, Algeria na mchakato wa amani nchini Sudan
Kusini.
Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa kwenye mkutano leo Ijumaa Mei 3,2019 jijini Johanesburg Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment