Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii Prof.Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawpo pichani) jana jijini Dodoma kuhusu namna ofisi yake
imejipanga kutumia jukwaa la mashindano ya AFCON U17 kutangaza fursa za
utalii zilizopo nchini katika kipindi cha mashindano hayo
yatakayofanyika hivi karibuni nchini, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi na Kulia ni
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred
Kidao.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akitoa shukrani kwa
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
kwa kutoa fedha kiasi cha Bilioni Moja za kuendesha mashindano ya AFCON
U17 yatakayofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam alipokuwa
akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dodoma,
Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda.
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dodoma kuhusu aina ya
wageni wanaotarajiwa kufika katika mashindano ya AFCON U17
yatakayofanyika nchini hivi karibuni ambapo alieleza Rais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino anatarajia kuja katika
mashindano hayo, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na
Utalii Prof.Adolf Mkenda.
………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – WHUSM- Dodoma.
Serikali ya dhamiria kutumia
jukwaa wa Mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika hivi karibuni
kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kunufaika na wageni
mbalimbali watakao kuja kushiriki michuano hiyo ya Kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda wakati wa
kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja
na
viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa lengo la
kuhakiki mikakati itakayotumika kutangaza vivutio hivyo ambavyo ni tunu
ya Taifa.
“Sisi Wizara ya Maliasili na
Utalii tutahakikisha tunatumia jukwaa hili la michezo kuongeza idadi ya
watalii katika vivutio vya utalii nchini na tumejipanga vizuri kwa
matangazo mbalimbali ambayo yanamvuto wa ushawishi kwa watalii hawa
wamichezo kuvutiwa kufika katika maeneo hayo tunafukwe nzuri,Mbuga za
wanyama,majengo ya kale yenye hishoria mbalimbali,maporomoko ya maji na
Mlima Kilimanjaro,”alisema Prof.Mkenda.
Akiendelea kuzungumza katika
kikao hicho Prof.Mkenda alisisitiza kuwa ujio wa mashindano hayo ya
AFCON U17 nchini ni jambo lenye manufaa makubwa kwa taifa kwani kwa
kujipanga vizuri huu ndiyo wakati wa kunufaika kwa watanzania wote
kupitia wageni hao, wajasiriamali mbalimbali watanufaika kwa namna moja
kwani wageni hao watahitaji huduma mbalimbali kwa kipindi chote watakapo
kuwa hapa nchini hivyo ni vyema watanzania watumie fursa hii.
Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi alitoa shukrani
kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya
kufanikisha mashindano hayo tunashukuru sana kwani fedha hizo zitasaidia
kukamilisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika kipindi cha
mashindano.
“Wizara yangu kama mlezi wa
Sekta ya Michezo Nchi mpaka sasa tumesha kamilisha mambo muhimu yote
tuliyoagizwa CAF na vimebaki vitu vidogo sana ambavyo vitakamilika ndani
ya muda mfupi hivyo naweza kusema tupo tayari kwa mashindano,”alisema
Bibi.Mlawi.
Pamoja na hayo nae Bibi.Mlawi
alieleza kuwa mashindano hayo yanataanza Aprili 14, Mwaka huu na Mechi
ya ufunguzi inatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam hivyo ni vyema wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na kujipanga kwa
ugeni huu na watanzania nivyema kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio
hili la kihistoria kwa taifa letu kuandaa mashindano haya ya Kimataifa.
Halikadhalika nae Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao alieleza kuwa katika
mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni
Infantino atakuja hivyo ujio wake katika mashindano hayo utakuwa ni
fursa ya kutangaza nchi yetu, vilevile uongozi wote washirikisho la
mpira wa Miguu Afrika (CAF) nao utahamia Tanzania katika kipindi chote
cha mashindano.
“Katika mashindano hayo ndipo
wadau wa soka duniani wanakuja kusaka vijana wenye vipaji kwa ajili ya
kuwaunga katika timu zao kubwa za kimataifa mfano mchezaji kama Neymar
ni mmoja ya wachezaji waliyoibuliwa katika mashindano ya mpira kwa
vijana chini ya umri wa miaka 17 hivyo wapo wadau mbalimbali duniani
watakuja kwa ajili ya hilo,”alisema Kidao.
Wito kwa watanzania ni kuwa
tayari kwa ujio huu wa kimataifa na kujipanga vyema kunufaika na wageni
hawa kwa kuhakikisha wanakuwa watulivu na wakarimu kwa ajili ya kuiletea
nchini mafanikio katika uchumi.
No comments:
Post a Comment