Waziri wa Madini Doto Biteko (wa
pili kushoto) akifuatilia hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wenyeviti wa kamati
nyingine wakati wa semina ya wabunge iliyotolewa na wizara. Wa pili
kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
Dustan Kitandula, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,
Prof. Simon Msanjila na kwa kwanza kulia ni Katibu wa Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Nishati na Madini, Omary Magwinza.
Waziri wa Madini Doto Biteko ( wa
kwanza kulia) akiandika jambo wakati wakifuatilia uwasilishaji mada ,
Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini, Dustan Kitandula. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Bunge ya Kudumu
ya Nishati na Madini, Omary Magwinza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula (kushoto) akiteta jambo na
Katibu wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Omary
Magwinza.
Waziri wa Madini Doto Biteko
(kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila
(Kulia) wakati wa semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati
nyingine wakifuatilia uwasilishaji wa mada uliotolewa na Wataalam kutoka
Wizara ya Madini na Taasisi zake.
Baadhi ya Watendaji na Wataalam
kutoka Wizara na Taasisi zake wakifatilia uwasilishwaji mada uliotolewa
na Wataalam wa Wizara ya Madini na taasisi zake.
Waziri wa Madini Doto Biteko na
baadhi ya Watendaji na Wataalam wa Wizara na Taasisi zake wakijadiliana
jambo baada ya kuhitimishwa kwa semina ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Nishati na Madni na baadhi ya Wenyeviti wa kamati nyinginr
iliyoandaliwa na wizara ya madini.
………………………
Imeelezwa kuwa, Wizara ya Madini
itaendelea kusimamia Uanzishwaji wa Masoko ya Madini katika maeneo
mbalimbali nchini huku ikiendelea kufanya marekebisho ya Kanuni za
Uanzishwaji wa masoko hayo.
Waziri wa Madini Doto Biteko
ameysema hayo Machi 31, 2019 wakati akifunga Semina ya siku mbili
iliyoandaliwa na wizara kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati zenye uhusiano
na Sekta ya Madini.
Semina hiyo ililenga kutoa elimu
na kujenga uelewa wa pamoja kwa wabunge hao kuhusu sekta ya madini
ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa.
Mada zilizowasilishwa ni pamoja na
uanzishwaji wa masoko ya madini, mafanikio na changamoto ya Shirika la
Madini la Taifa STAMICO), elimu kuhusu majanga ya asili (hasa matetemeko
ya ardhi), ukaguzi migodini, biashara ya madini na shughuli
zinazofanywa na Taasisi ya Uwazi na uwajibikaji katika Rasiimali za
Madini, Mafuta na Gesi Asilia.
Waziri Biteko aliongeza kuwa,
Wizara itaendelea kuwaelea wadau wa madini huku akiwataka kubadilika na
kutenda matendo yenye manufaa kwa pande mbili na kuwaomba wabunge hao
kushirikiana na serikali katika kutoa elimu kwa wadau wa madini ili
waweze kuzingatia na kufuata taratibu zilizowekwa.
Pia, alisema serikali itaendelea
kufanya kaguzi migodini kwa lengo la kuhakikisha wachimbaji wanachimba
kwa usalama na kueleza kuwa, wizara imeomba kibali cha kuongeza maeneo
mengine ya ukaguzi wa madini na kusema,“ tumepanga kuongeza vituo
vingine 85”.
Aidha, alizungumzia maeneo yenye
wizi wa dhahabu katika maeneo ya kuchanjua madini hayo na kuyataja kuwa
ni Kahama na Chunya na kuwataka wahusika kuzingatia sheria na
Akizungumzia suala la kupunguza
zaidi kodi kwa uchimbaji mdogo wa madini, alisema serikali haitapunguza
tena kodi hizo kwa sasa mpaka hapo itakapoona manufaa yake.
Ikumbukwe kuwa, baada ya mkutano
wa Kisekta uliofanyika Januari 22 mwaka huu chini ya Uenyekiti wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli na kuwashirikisha
wadau mbalimbali wa madini baada ya wadau hao kuwasilisha kero zao kubwa
ikiwa kodi, serikali ilifanya mabadiliko na kuondoa kodi kwenye
uchimbaji mdogo wa madini kwa kuwafutia kodi ya ongezeko la thamani
yaani VAT (18%) na kodi ya zuio( withholding tax).
Mbali na wajumbe wa kamati,
wengine walioshiriki semina hiyo ni Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo
chini ya Wizara pamoja na Watendaji na Wataalam kutoka wizara na taasisi
zake.
No comments:
Post a Comment